KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, July 25, 2015

WAGONJWA 1000 WAPEWA CHAKULA NA WAISLAMU SONGEA


Waumini wa Kiislamu na Madhehebu mengine wametakiwa kuwa na huruma kwa kusaidia watu wenye shida wakiwemo maskini, wafungwa na wagonjwa waliolazwa Hospitalini.


Katibu wa Msiki wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Mohamed Mfyule ameyasema hayo wakati akigawa chakula kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wapatao 1000. 


Katibu wa Msiki wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Mohamed Mfyule
amesema wakati wa Siku ya sikukuu mbambali  ni wajibu wa Waumini  wa Dini mbalimbali kufanya Hija katika Hospitali kwa kuwaona  Wagonjwa waliolazwa na kuweza  kuwafariji hiyo nayo ni ibada

Wagonjwa akila chakula baada ya waislamu kuwa gawia katika kusherekea sikukuu ya idi
Akina mama waja wazito wakijipatia chakula katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma
P0amoja na sherehe ya sikukuu ya iddi waisilamu walijitolea kushinda hospitali
Wagonjwa wapatao 1000 mwakijipatia chakula na kuwaombea waisilamu waendelee na moyo huo huo
Ukiwa siyo mzazi huwezi kujua uchungu wa mimba pamoja na waislamu kujitolea kupeleka chakula lakini akina mama hawa wana sema chakula hakinogi wanaomba waislamu wawaqombee ili wajifungue kwa haraka
Waislamu wakiendelea kutoa chakula huku wakiwafariji waja wazito
muguzi mama mbawala akiwa wodini ,hapo ana washukuru waislamu kwa kutoa chakula na kuwaomba madhehebu mengine waige mfano huo
kweli moyo wawaumini upo kwenye matatizo ndivyo inavyo dhirisha katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma
Unapo sherekea sikukuu ni lazima ujue niviumbe vingapi vina kutegea hapo paka akiwa ameshiba baada ya kupewa chakula
                   Katibu wa Msikiti wa Hospitali akisimamia kwa makini mtu asikose chakula
                  Mambo hayo hapo ni kula tu waislamu wana fanya kazi
Waumini mbalimbali waliokuja kuwaona wagonjwa wao  nao wameshukuru moyo ulio onyeshwa na Waislamu kwa  kujitolea kutoa chakula kwa wagonjwa 1000 


Wagonjwa mbalimbali waliolazwa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wamewaomba wa watu mbalimbali kuja kutoa misaada kwa wagonjwa kwani wako wagonjwa wengine ambao hawana ndugu.  Nao wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma  wamewashukuru  waislamu kwa kuweza kutoa  msaada wa  chakula  kwani chakula ni dawa  ikiongozana na ufariji wao wagonjwa .

No comments:

Post a Comment