KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, March 12, 2016

MFANYAKAZI WA HOSPITALI YA MKOA WA RUVUMA BENEDICT MLAPONI APOTEA YAPATA MIAKA 10 SASA


 Nimtoto wa Benedict Mlaponi ambaye amebaki kama yatima Emanuel Mlaponi ambaye yuko kidato cha pili hana Mbele wala Nyuma baba yake alitoweka mwaka 2005 .Mirasi ili funguliwa na serekari kuridhia watoto hao pamoja na mama yao kupewa mirathi hiyo sasa hatujui kama ilichukuliwa au ndiyo majipu yanayo tumia Fedha za wajane .Mheshimiwa Rais wangalie Watoto hawa ili waende na kauli ya Hapa kazi
Mtoto Emanueli Mlaponi na Mama yake Mzazi   wakiomba msaada kwa Rais wa Jamuhuri ya Mungano Mh,John Pombe Magufuli kuangalia masilahi ya mirathi ya baba yao ambaye alikuwa mtumishi wa umma katika Hospitari ya Mkoa wa Ruvuma, Mirathi ili pita lakini mpaka sasa familia hii ina endelea kuhangaika hajulikani fedha ime ingia mikononi mwa majipu au kutokana na mtui wakufuatilia hana uzito. Mh.Rais Ingilia kuisaidia Famila hii ili ijulikane serekari ipo
Ndugu Mtazamaji i unayemuona hapo juu anaitwa  Benedict Mlaponi  alikuwa Mfanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Alipotea toka 13/10 /2005 mpaka leo hajulikani aliko. 

Mara ya mwisho aliaga kuwa anasafiri kikazi Dar es salaam na alipata Ruhusa kutoka kwa Mkuu wake wa kazi Dr Wella kwa wakati huo, toka wakati huo mpaka leo 2016 hajapatikana na haijulikani kama yuko hai au amekufa.
Benedict Mlaponi ameacha watoto 5 na Mke Angetruda Milinga,  Masikini wa Mungu Benedict Mlaponi  kazini alikokua ameajiriwa bila kujua lililompata wakaandika barua ya kumfukuza kazi.  Mkewe Angetruda Milinga alifungua kesi ya mirathi baada ya kutoa ripoti police na kuona hapatikani Mahakama ikaamuru alipwe fedha ya mirathi lakini Serikali ya Mkoa wa Ruvuma haija weza kufanya hivyo. 
Ombi la Mke na familia kwa watanzania Mumewe alikuwa akifanya kazi Serikalini kwa nini asilipwe mafao ya mirathi wakati kesi ilishapitia na kuthibitika mumewe kafariki kwa mazingira ya kutatanisha.

 Mwisho anamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumsaidia mjane huyu kwa kuwa sasa ana tegemea nguvu ya Rais ikishindikana aombe uwezo wa Mungu

No comments:

Post a Comment