KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, June 25, 2016

MGOMBEA UBUNGE KUPITIA CHADEMA ATAKIWA KULIPA GARAMA ZA UCHAGUZI SHILINGI 12,395,000/=


Mahakama Kuu Kanda ya Songea imetoa hukumu Kesi ya Madai ya Gharama za Kesi ya Uchaguzi dhidi ya Joseph Fyime na Leonidas Gama ya Madai ya Shilingi Milioni `13 aliyotakiwa kulipwa Leonidas Gama.
Msajili wa Mahakama kuu Kanda ya Songea George Herbert amesema ametoa hukumu hiyo baada ya kuangalia hali halisi ya uendeshaji wa Kesi ya Madai dhidi ya ndugu Joseph Fyime  ambaye alikuwa akidaiwa alipe gharama ya shilingi Milioni 13,000,000/kwa ajili ya garama za uchaguzi lakini mahakama kuu imemwamuru joseph Fyime wa chadema kulipa shilingi milioni 12,000,000./= kukidhi garama hizo


MAHAKAMA KUU KANDA YA SONGEA IMEMALIZA KESI DHIDI YA ALIYEKUWA MGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA NA ALIYESHINDA UBUNGE JIMBO LA SONGEA KWA KUMUAMURU MGOMBEA WA CHADEMA ALIPE GHARAMA ZA UENDESHAJI WA KESI YA UCHAGUZI. TS. 12,395,000/=Mgombea Ubunge kupitia Chama cha CHADEMA Joseph Fuime amesema kutokana na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu  ya  Songea ya kumtaka alipe Milioni 12,395,000 ameipokea na anaangalia jinsi ya kuitekeleza kama ataweza kukata rufaa.
Mgombea Ubunge kupitia CHADEMA Joseph Fuime amesema Chama chake cha CHADEMA toka Kesi imeanza mpaka imeisha kimeshindwa kutoa msaada na hali hiyo siyo yeye tu hata wengine walio na kesi za uchaguzi hakuna aliyesaidiwa hiyo ni kukatisha Tamaa wanachama.

No comments:

Post a Comment