KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, June 25, 2016

WATU WAWILI WAME FARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA DALALALA KATIKA MANSPAA YA SONGEA


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Songea Daktari Philp   Nyimbi amesema  walipokea maiti moja ya mtu ambaye alikuwa anatembea kwa mguu nan kugongwa na gari  jina lake halijafahamika anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 - 25 ambaye alifariki mara baada ya kugongwa  na Majeruhi mmoja mwendesha pikipiki aliyetambulika kwa jina la Frenk Mahundi mkazi wa lizaboni ambaye alifikishwa katika Hospitali ya Mkoa kutokana na kupoteza damu nyingi alifariki  wakati akiendelea na matibabu


Watu wawili wamefariki Dunia baada ya kugongwa na Basi la Daladala lenye namba za Usajili T811 AHG lililokuwa likitoka Songea kwenda Kwenda Hospitali ya Misheni ya Peramiho.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Songea Daktari Philp   Nyimbi amesema watu hao ambao waligongwa katika eneo la Mkoni Manispaa ya Songea wamefariki baada ya kutokwa na Damu nyingi baada ya Ajali.Nao wananchi walioshuhudia ajali hiyo wamesema ajali  hiyo iliitokana na mwendo wa  kasi  hivyo dereva  alishindwa kuliongoza gari hilo na kuwa gonga watu wawili kwa mpigo      
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombezi amesema vifo vya watu hao wawili vilitokana na Mwendo  wa kasi, Jeshi la Polisi linamtafuta Dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo ambaye ametoroka baada ya kusababisha ajali.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma  Zuberi Mwombezi  amewaomba wananchi  kuwa inapotokea Ajali wawahi kuwakimbiza Majeruhi Hospitali  badala ya kusimama na kuwa shangaa

No comments:

Post a Comment