KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, June 25, 2016

SERIKALI IMESEMA IMEHAIRISHA KWA MUDA AJIRA MPYA, AJIRA MBADALA NA MAREKEBISHO MBALIMBALI YA WATUMISHI KUTOKANA NA KUPISHA ZOEZI LA UHAKIKI WA WATUMISHI HEWA ILI KUPATA TAARIFA SAHIHI ZA WATUMISHI WAKE.


Katibu Mkuu wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma Daktari Lauren Ndumbaro amesema shabaha ya Serikali kuendesha Zoezi hili ni kutaka kuwadhibiti wale ambao wanapokea mishahara bila kufanya kazi na kujenga Muundo bora wa uongozi katika Serikali hii ya awamu ya tano.
Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma Daktari Lauren Ndumbaro amewatoa wasiwasi watumishi kuwa kufanyika kwa mazoezi hili  si kwamba watumishi watapoteza haki zao laa, baada ya uhakiki kukamilika mambo yatarudi kama kawaida.


Serikali imeamua kuhairisha Ajira Mpya, Ajira mbadala, Upandishaji wa Vyeo pamoja na Marekebisho ya nyongeza za Mishahara mpaka zoezi la Uhakiki wa Watumishi hewa litakapokamilika.
Katibu Mkuu wa Utawala Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Daktari Lauren Ndumbaro ameyasema hayo wakati akizungumza na Watusmishi wa Halmashauri tatu za wilaya ya Songea kuhusu zoezi la uhakiki wa watumishi Hewa.


Watumishi wa Umma katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameomba Serikali kuangalia Upya kwani wapo watumishi ambao wanafanya kazi Serikalini wanafikia miaka miwili bila kupata mishahara na wengine wanafikia mwaka hawajapandishwa vyeo wala kuongezwa mishahara baada ya kusoma.


Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma Daktari Lauren Ndumbaro amewataka watumishi wote wanaoidai Serikali katika nyanja mbalimbali kuwa wavumilivu  wakati Serikali ikiendelea kufanyia kazi Masuala yao. 

No comments:

Post a Comment