KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, October 25, 2016

KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI AINA YA URAN YA NAMTUMBO YATOA VIFAA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 12 KWA DAWATI LA POLICE WANAWAKE RUVUMA

 Mwenyekiti wa Dawati la Police Wanawake Anna Tembo akisoma Risala ya Mafanikio na Changamoto inalo li kabili Dawati la Jinsia Mkoa wa Ruvuma kwa Kukosa Vitendea Kazi
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge pichani akipokea vifaa vilivyoahidiwa na kampuni ya Mantra inayomilikiwa na kampuni ya Rosatom ya Urusi ambayo inahusika na uchimbaji wa madini ya uran Mkuju wilayani Namtumbo wametoa aseti za seti nne ya viti,  meza za kisasa Kompyuta,  photocopy mashine, scana, printer, TV Flat Screen,  kamera, kaunta ya vioo vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 12
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Akipokea msaada wa Vifaa kutoka kwa Afisa Mahusiano wa Mantra Khadija Pallangyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Kampuni iliyotolewa na MANTRA chini ya Kampuni ya ROSATOM ya Urusi.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge akisalimiana na Mwenyekiti wa uhamasishaji kupinga ukatili wa kijinsia mkoa wa Ruvuma ndugu Mkude katika viwanja vya jengo Dawati la Police wanaewake Mkoani Ruvuma.
 Mkuu wa kituo cha police wilaya  ya Songea akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mara alipo tembelea Dawati la Jinsia la Police Mkoa wa Ruvuma
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge  ametoa angalizo kwa jeshi la Police kuhakikisha Dawati la Police Wanawake lina kuwa  na wataalamu wanao wiana na umahiri wakuweza kutatua matatizo yanayo ikabili jamii kwa kuweka watu wenye umakini wa kufanya kazi kwa kulinda heshima na utu wa mtanzania na sio kuweka mtu yeyote ili mradi Askari pasipo kujali uwezo wake
 Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma ACP Zuberi Mwombeji ameahidi mbele ya mkuu wa mkoa kutoa wataalamu wenye uwezo kushugulikia dawati kwa umakini na usiri kutegemea cheocha mtu aliye kwenye dawati huku akizingatia uwezo alio kuwa nao katika kusaidia jamii.

 Mwenyekiti wa kamati ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya jamii ya watanzania Renatus Martias Mkude alinukuu suala la maendeleo yaliyo tolewa na Rais Benjamini Wiliam Mkapa wa awamu ya tatu kuwa jambo jema linalo anzishwa na mtu mmoja ni budi liungwe mkono na watu wengine ili liweze kuletaufanisi na maendeleo kama hili linalofanywa na Dawati la Police katika kupinga ukatili wa kijinsia miongoni mwa jamii.
 Mwenyekiti wa kamati ya kupinga ukatili wa kijinsia bwana Renatus Martias Mkude akiainisha mafanikio yaliyopatikana katika kuhdumia watu walio athirika na vitendo vya ukali wa kijinsia, pamoja na mama aliyekuwa anaishi Peramiho ambaye alijichongea jeneza lililovunjwa na kamati ya kupinga ukatili wa kijinsia, lakini hatimaye mama huyo wiki mbili zilizopita alifariki ambapo na kamati iliweza kuchonga sanduku lingine na kumzika mama kwa ushirikiano na wananchi wa Pearamiho
 Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema utafika wakati wa kuchimba madini yaliyopo Aridhini pale tutakapowapata watanzania ambao wanaweza kusimamia na kuelekeza madini hayo ya saidie wananchi wote, Ndivyo alivyofanya dada Khadija Pallangyo kwa kusimamia kampuni ya Mantra inayomilikiwa na Kampuni ya ROSATOM ya Urusi inayochimba madini ya uran na faida inayopatikana ikilenga kusaidia jamiii inayozunguka Maeneo ya igodi. MANTRA imekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 12 chini ya Afisa Uhusiano Mzalendo Khadija Pallangyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Bilinith Satano Mahenge akisikiliza taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Dawati la Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo iliyoainisha hali ya vitendo vya ukatili mkoani Ruvuma
 Hivyo ni vifaa vilivyotolewa na Kampuni ya MANTRA yenye makao yake makuu wilaya ya Namtumbo katka mgodi wa Urenium One Mkuju
                                                  sehemu ya vifaa vilivyokabidhiwa
Vifaa kama vinavyoonekana hizo ni Sacana na Printa
 Wadau mbalimbali waliohudhuria katika makabidhiano ya vifaa vilivyotolewa kwaDawati la jinsia la Police wanawake ili kurahisisha utendaji wa kazi za dawati. Kutoka kushoto ni Mussa Homera na kulia kwake ni Mratibu mhamasidhaji wa ujenzi wa jengo la dawati Bw. Juma Nyumayo
 Mdau mkubwa wa Dawati la jinsia Frenk Mchina akiwa wadau wengine akiwemo Mr Zuberi ambao wameshiriki kwa karibu katika kuchangia masuala mbalimbali ya dawati la jinsia la polisi hapo wakifuatilia utoaji wa vifaa vitakavyosaidia utendaji kwa jamii ya wana Ruvuma
 Mhamasishaji maarufu mkoani Ruvuma Meki Mguhi akiendesha mapokezi ya vifaa kutoka Kampuni ya Uranium one
 Kamati ya ulinzi na usalama wakishuhudia vifaa vikipokelewa baada ya kutolewa na MANTRA
 wadau mbalimbali wa Mkoa wa Ruvuma wanaounga mkono Dawati na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia Mkoani Ruvuma
 Kutoka kushoto ni kamanda wa Police Mkoani Ruvuma ACP Zuberi Mwombeji na katikati Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge
 Picha ya Pamoja kati ya Dawati la Police Wanawake na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Binilith Satano Mahenge
 OCD na Mwenyekiti wa Dawati la kupinga ukatili wa kijinsia Anna Tembo wakipongezana kwa kuendesha Dawati la Police Wanawake
 Mwenyekiti wa kamati ya kupinga ukatili Mkoa wa Ruvuma Mkude akisalimiana na Mwenyekiti wa Uhamasishaji wa Jengo la Police Wanawake Adamu Mzuza Nindi ambaye pia ni mkurugenzi wa Blog ya Songea Habari
 Khadija Pallangyo akiwa katika Viwanja vya Police muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa kwa Dawati la Jinsia la Police Wanawake Mkoani Ruvuma.
 Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando amesisitiza utoaji wa huduma kwa watu wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ameomba kamati ya ulinzi na usalama kushiriki kikamilifu katika kusimamia suala hilo
 Kamati ya Ulinzi na usalama wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge
 Sehemu ya Caunter ya Dawati la Police wanawake ambayolimejengwa na kampuni ya uchimbaji wa Madini ya Uran One machimbo yaliyoko Mto Mkuju wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma

No comments:

Post a Comment