KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, October 16, 2016

WAKALA WA MISITU KANDA YA KUSINI WATOA MADAWATI 580 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 43


Wakala wa Misitu Kanda ya Kusini wameweza kutoa Madawati 580 katika Shule za Msingi za Mkoa wa Ruvuma, Madawati hayo yakiwa na thamani ya shilingi Milioni 43.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akiwa na wanafunzi wa shule ya majiamaji akiwa uliza maswali  

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema ili kufikia uchumi wa kati, ni lazima kuimarisha miundo mbinu ya Elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha Eneo la Kusomea kuwa na Walimu wenye wito, wazazi na Serikali kushirikiana kulinda Miradi ya Elimu

Wanafunzi waliopewa Madawati  wameweza kushuuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka mikakati ya kuweza kuwafanya wanafunzi wasikae chini waweze kusoma vizuri.


Afisa Elimu Manispaa ya Songea amewaomba wazazi na Wanafunzi kulinda Madawati yaliyotokana na wadau ili Madawati hayo yaweze kudumu kwa Vizazi vingi.

Mkoa wa Ruvuma kwa kiasi kikubwa wameweza kufikia lengo la asilimia 99 ya watoto kukaa kwenye Madawati. Vita iliyopo kwa sasa ni kuhakikisha watoto wanatumia vyoo bora vyenye hali ya kisasa pamoja na kuwa na Benki ya Tofali ili kukiwa na kazi yoyote ya Ujenzi tofari hizo ziweze kutumika.

Viongozi waliohudhuria zoezi la kukabidhi adawati 580 kutoka kwa wakala wa Misitu kanda ya kusini katika Ukumbi wa Maliasili Mkoani R
mshauri wa kisheria Fatuma Misango akieleza changamoto zinazo mpata mtoto wa kike
mtalamu wa mbegu za nafaka kutoka katavi  Joanthan akitoa elimu ya jinsi ya kutumia mbegu za kisasa
Mtalamu wa mbegu kutoka katavi akitoa elimu mbegu zinazo faa koa wa ruvuma ambazo zime fanyiwa utafiti wa kutosha

Kaimu Meneja wa Wakala wa Misitu Kanda ya Kusini Embrantino Mgiye amesema pamoja na kutekeleza Amri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwataka wanafunzi wote wa Shule za Msingi na Sekondari kuwa asiwepo mwanafunzi wa kukaa chini lakini Wakala wa Misitu wameona ni vyema Wananchi wafaidi Rasilimali zao kwa kutoa Madawati kwa Wanafunzi ili tupate wataalamu wazuri kwa kukaa watasoma kwa utulivu.

Kaimu Meneja wa Wakala wa misitu Kanda ya Kusini amesema utoaji wa madawati kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari ni somo tosha la kuwawezesha wanafunzi  kujua kumbe misitu inasaidia kila mtu hivyo wanafunzi  wataweza kukua na kujua faida  za misitu.
mkurugenzi wa manspaa ya Songea akiwa na katiu tawala wilaya ya Songea Pendo wakati wamakabidhiano wa madawati kutoka kwa wakala wa hifadhi ya misitu kanda ya kusini

No comments:

Post a Comment