KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, October 31, 2016

UTAFITI WA HALI YA MAAMBUKIZI YA VVU NA UKIMWI NCHINI TANZANIA KUFANYIKA KWA TEKNOLOJIA YA KISASA


Jumla ya watu 35,000 hufa Nchini Tanzania kutokana na Maambukizi ya VVU na UKIMWI na watoto 600,000 huachwa katika hali ya uyatima kila mwaka.


Akisoma Taarifa ya Takwimu za maambukizi ya UKIMWI  kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr. Binilith Satano Mahenge  amesema Takwimu ni kubwa hivyo ili kuweza kupunguza ongezeko  hilo  inabidi kutumia njia shirikishi itakayo kuwa na idadi sahihi ya maambukizi 

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Mihayo Bupumba amesema njia ya kwanza ni kuhakikisha wale wote walioathirika wanajulikana kwa asilimia 90%, njia ya pili ni kutambua kama hao walioathirika wanapata dawa za ARV kwa asilimia 90%  njia nyingine ni kufahamu na kudhibiti maambukizi mapya kwa asilimia 90% kwa kufanya sense ya kitalamu bila kumlazimisha mtu

 Katika utafiti huo Mkoa wa Ruvuma utahusisha katika wilaya zote kinachotakiwa ni wale wanaotakiwa kuwakilisha kushiriki kikamilifu.
 Wadau wa Mapambano dhidi ya ukimwi kutoka halmashauri za Mkoa wa Ruvuma, Taasisi za Dini na Asasi zinazoshughulika na masuala ya UKIMWI wakiwa katika mkutano wa kupokea taarifa ya Utafiti wa Viashiria vya Ukimwi unaotarajia Kufanyika Tanzania nzima kwa kaya wakilishi.
 Wadau wamesisitizwa kutoa ushirikiano katika zoezi hilo muhimu ili kufahamu Takwimu sahihi za hali ya maambukizi zitakazosaidia Serikali kujua namna ya kupanga Bajeti katika kuhudumia waathirika wa VVU
 Wataalamu wa Afya kutoka Kitengo cha Utafiti wa Viashiria vya VVU na UKIMWI
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma akitoa taarifa ya namna walivyoandaa maeneo yatakayohusika na utafiti huo kwa kushirikiana na waratibu na watakwimu.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino Mihayo M. Bupamba akielezea teknolojia itakayotumika katika utafiti kwa kutumia electronic ambayo itatoa usahihi wa data.

No comments:

Post a Comment