KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, October 26, 2017

MTAMBO WAKISASA WA HALI YA HEWA WAFUNGWA MKOANI RUVUMA


Mradi wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na mifumo Awali, imetumia shilingi bilioni 2.9 kwa ajili ya kufunga Mitambo ya Hali ya Hewa Nchini Tanzania KATIKA VITUO 36.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera Bunge Ajira na watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema katika Bara la Africa ni Nchi mbili pekee zimeweza kufunga mitambo ya kisasa ya kukabiliana na Majanga ya Mabadiliko ya hali ya hewa nazo ni Tanzania na Ephopia.


Mratibu wa kitaifa wa uboreshaji wa Hali ya Hewa Nchini Tanzania Alfei Daniel amesema mitambo hiyo ya Hali ya Hewa sasa imeunganishwa na simu kwa wakulima ili waweze kufaidika na matumizi ya Kilimo pamoja na kuepukana na Majanga mbalimbali, Naye Brigedia Jeneral Mbazi Msuya amesema Tanzania imesonga mbele katika kukabiliana na Majanga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera Bunge Ajira na watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akiwaeleza faida za kuwa na mtambo wa kisasa na faida itakayo patikana katika shule za msingi na sekondari,vyuo vikuu vilivyo jirani na mtambo kujifunza kwa nadharia



Mh. Jenista amesema mitambo hiyo kwa sasa iweze kufanya kazi zaidi kwa kutoa ELimu katika Sekondari kwa kufundisha wanafunzi somo la Jiografia ili kuongeza ufahamu katika kukabiliana na majanga mbalimbali.


Mitambo ya kujua Masuala ya Hali ya Hewa imefungwa katika Vituo 36 kwa Tanzania na mzima na kusababisha kuboresha taifa sahii kutoka asilimia 82% hadi kufikia asilimia87%  waziri jenista amesema elimu ya kujua hali ya hewa ina takiwa kila Halimashauri iwe na watu wanao toa tarifa                                                                                                     

Brigedia Jeneral Mbazi Msuya akielezea mafanikio ya ufungaji wa Mitambo ya Hali ya hewa jinsi yanavyo waokoa wakulima ,Wakulima zaidi ya miambili wame pewa simu ili kwenda sambamba na utabiri wa hali ya hewa
mhandisi TMA David Chilambo akimwelezea Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera Bunge Ajira na watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagamajinsi mtambo huo wa hali ya hewa unavyo fanya kazi kwa haraka na kuweza kujua tatizo lolote likitokea linalo husu Majanga
Vijana wako tayari kupambana na majanga yanayo tokea kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa hapo Mhandisi David Chilambo akimweleza kwa makini Mh, Jenisa kuhusu mitambo inavyo fanya kazi mtambo mmoja hugharimu kiasi cha shilingi milioni 78 kwa fedha za kitanzania

No comments:

Post a Comment