KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, April 10, 2018

BUSTANI YA MANISPAA YA SONGEA KUANZA KUTUMIKA MWEZI MAY 2018


MRADI wa bustani ya Manispaa ya Songea umekamilika unatarajia kuanza kufanyakazi mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, ambapo Mkandarasi tayari amekabidhi mradi huo kwa Manispaa.

Kaimu Mkuu wa Idara ya ujenzi wa Manispaa ya Songea Mhandisi Nicolus Danda amesema mradi ulikamilika tangu Desemba 2017 ambapo Mkandarasi alipewa matazamio ya miezi sita ya mradi huo  ambayo inaishia Aprili 2018.


Mradi wa Bustani ya Manispaa ya Songea umejengwa kwa ufadhili na Benki ya Dunia kwa  gharama ya shilingi milioni 399, hadi kukamilika mradi umetumia shilingi milioni 444.

Wawakilishi  wa Benki ya Dunia wameukagua mradi huo na kuridhishwa na kiwango cha ujenzi wake na kusema Bustani hiyo  imebadilisha muonekano wa mji wa Songea.
Mradi wa Bustani ya Manispaa ni miongoni mwa Miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya Mpango wa Kuzijengea uwezo serikali za mitaa (ULGSP).

Ujenzi wa Bustani hiyo umehusisha eneo la mgahawa, choo cha kulipia, uzio, maeneo ya kupaki magari(parking bay), eneo la kupumzikia(resting huts) na maeneo ya kuchezea watoto,  Pia kwa siku za baadaye bustani hiyo inatarajia kuwa na kituo cha kutolea Habari za Utalii na uwekezaji ndani ya Manispaa na Mkoa wa Ruvuma

No comments:

Post a Comment