KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, April 12, 2018

WAKALA WA MAJENGO TBA IMEKABIDHI MABWENI MATATU NA MADARASA MAWILI YA WASIOONA SONGEA


WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) wamekabidhi mabweni matatu na madarasa mawili ya shule ya msingi Luhira iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi huo na Manispaa ya Songea, Meneja wa TBA Mkoa wa Ruvuma Edwin Nunduma amesema mradi huo ulihusisha ujenzi wa mabweni matatu na ukarabati wa madarasa mawili kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 151
Kwa mujibu wa Meneja huyo wa TBA kila bweni Lina uwezo wa kulaza wanafunzi 12 hivyo mabweni matatu yatalaza wanafunzi wenye ulemavu 36.

Mkuu wa shule hiyo Joyce Konga ameishukuru serikali kwa kuwajengea mabweni ya kisasa na kukarabati madarasa mawili ambayo pia yana Mazingira rafiki kwa wenye ulemavu,  amesema shule ya msingi Luhira ina jumla ya wanafunzi 48 wenye ulemavu na kwamba baadhi ya wanafunzi wenye umri mdogo watalazimika kulala wawili wawili.

Shule ya msingi Luhira ndiyo Shule pekee yenye kitengo cha wasioona mkoani Ruvuma ambayo ilianzishwa mwaka 1929 na kitengo cha wasioona kilianzishwa mwaka 1982

Shule ya msingi Luhira ina jumla ya wanafunzi 1300 kati yao wenye ulemavu ni 48.Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme alitembelea shule hiyo na kukabidhi magodoro 24 yenye thamani ya shilingi milioni 1.8 kwa ajili ya wanafunzi wasioona wanaosoma katika shule hiyo.

No comments:

Post a Comment