KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, April 10, 2018

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA SONGEA KUTEMBELEA UJENZI WA MACHINJIO YA KISASA KATA YA TANGA MANISPAA YA SONGEA


 Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ametembelea MRADI wa machinjio ya kisasa unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni tatu unaotarajia kukamilika kabla ya Juni 30 mwaka huu.
 Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Songea katika kukagua Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa inayojengwa kata ya Tanga manispaa ya Songea.
Mradi huo unaojengwa katika kata ya Tanga Manispaa ya Songea kwa sasa umefikia asilimia 80 ya ujenzi wake, Mkandarasi wa ujenzi ujenzi huo Kampuni ya Giraffe ameahidi kukamilisha ujenzi wa machinjio hiyo kabla ya tarehe ya mwisho wa mkataba ambapo mkataba wa ujenzi ulianza Julai 2017 na kukamilika Julai 2018.
Manispaa ya Songea imekuwa ikijitahidi kuboresha huduma mbalimbali za wananchi ili kusogeza huduma karibu na wananchi Machinjio ya kisasa inayojengwa Kata ya Tanga itasaidia kuongeza Mapato ya Halmashauri ya Manispaa itakapoanza kutumika.
Muonekano wa Majengo ya Mradi wa Machinjio hali ilivyo kwa sasa, Wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika biashara ndogo ndogo katika eneo hilo la Machinjio pindi mradi utakapokamilika.
Ujenzi wa Machinjio ya kisasa unavyoendelea katika Kata ya Tanga Manispaa ya Songea.

No comments:

Post a Comment