KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, June 3, 2013

CCM MKOA WA RUVUMA WATAKIWA KUACHANA NA UBINAFSI KATIKA CHAMA CHA MAPINDUZIKatibu mkuu wa CCM Taifa Abdurahamani  Kinana  amewataka wana CCM kuacha tabia ya ubinafsi ambayo inaleta mfarakano ndani ya chama cha Mapinduzi.
Katibu mkuu wa chama Tawala cha CCM Taifa ameyasema hayo wakati akifungua semina ya mabalozi wa manispaa ya songea wapatao 4297 semina iliyo fanyika uwanja wa majimaji songea.Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM  Taifa Emanuel John Nchimbi amewataka wana CCM kuwa na Tahadhari na watu wanaotaka kuigawa Nchi kwa kutumia Ukabila au Dini akitoa Mfano wa Meseji zinazosambazwa amesema, "kuanzia jiwe la  mzungu hadi kilwa mto msimbati  mpaka ulipo ishia mto Ruvuma hadi bahari ya hindi ina faa kuitwa Tanzania ya kusini, mbona wenzetu Sudani  wamefanikiwa kujitenga mwisho wa kunukuu". Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Emanuel John Nchimbi amewaomba wana CCM kuji epusha na uchochezi huo;Katibu mkuu wa CCM Taifa Abduramani Kinana amesema CCM imegundua kuwa chama cha mapinduzi kina pendwa na watu wengi  isipo kuwa baadhi ya watu katika chama  hupandikiza watu wasio kubalika ndiyo maana jimbo la songea lili weza kupoteza viti 6 vya Udiwani. Katibu mkuu wa CCM Abdurahamani Kinana amewataka wana CCM kuachana na tabia za ubinafsi kuchagua  kwa kusema huyu ni mwenzetu mtindo huo uachwe mara moja

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi  Mkoa wa Ruvuma akitoa Tarifa kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdurahamani Kinana katika ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma
Wajumbe wa Kamati kuu ya CCM Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika uwanja wa Majimaji wakati wa semina kwa Mabalozi wa CCM Manspaa ya Songea


Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma kimepoteza Viti zaidi ya 6 kwa sababu ya Ubinafsi kwa kujali maslahi ya mtu mmoja mmoja kuliko kujali Maslahi ya Watu wengi na walio wengi kusema bora tupoteze  ili tukose Wote

Msanii wa Kikundi cha Maiko Jacksoni akionyesha alivyo fufuka na chama cha Mapinduzi katika onyesho maalum kwa Katibu mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdurahamani Kinana
Msanii wa Kikundi cha Maiko Jacksoni akiwa ndani ya Jeneza katika uwanja wa Majimaji Songea huku moto ukiunguza jeneza hilo lakini alipo fufuka akatoa kauli amefufuka na Chama Cha Mapinduzi

No comments:

Post a Comment