KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, August 15, 2015

RUVUMA PRESS CLUB YAPATA VIONGOZI WAPYA JEE KUSONGA MBELE KUTA KUWA NA UWEZEKANO AU TUTEGEMEE NINI WOTE TUFUATILIE


Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club Andrew Kuchonjoma amewataka waandishi wa Habari kuwa na umoja katika mambo mbalimbali, pia amewataka Waandishi kujiendeleza katika Elimu.


Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma (RPC) Andrew Chatwanga amewataka Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma kuimarisha Vitega Uchumi ikiwa ni pamoja na kuanzisha Redio pamoja na kujenga Ofisi na Nyumba za kulala wageni. Mradi wa Redio mpaka kukamilika unahitaji shilingi Milioni 25.


Katibu Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma, Ngaiwona Nkondora ameombwa na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma kuwa mvumilivu na mtulivu katika kutekeleza masuala ya klabu ya waandishi wa habari wa Ruvuma Press Club (RPC)


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma Marietha Msembele amewataka waandishi wa habari kushirikiana naye katika Uongozi, hakuna kitu ambacho kiongozi peke yake anajua.


Mweka hazina Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma Alpius Mchucha ameomba kupewa ushirikiano na waandishi katika kutekeleza majukumu yake.


Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Ruvuma Press Club wametakiwa kuwasukuma Viongozi wa ngazi za juu ili walete Maendeleo ndani ya Chama cha Waandishi wa habari.

Wajumbe waliochaguliwa katika Kamati ya Utendaji ni, Kassian  Nyandindi, Mpenda Mvula,Geofrey Nilahi, Joseph Mwambije na
 Mpenda Mvula kiongozi wa Kamati ya Utendaji sijui ana fikilia kupiga Mzinga Gani bora afikili e Maendeleo

Picha hiyo ni Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Ushirika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Ruvuma Press Club wakiwa na Furaha baada ya kuwapata Viongozi

Picha hiyo ni Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Ushirika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

                   Mwandishi Andrew Mwaiki akiwa kwenye uchaguzi jengo la ushirika songea
Mwandishi Cerencesia Kapinga ambaye alikuwa katika kamati ya Utendaji kwa hivi sasa hakugombea kutokana na Jukumu la kugombea kata ya Ndirima Litembo hapo October 25 Mwaka huu

No comments:

Post a Comment