KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, August 1, 2015

WAKULIMA WA NYANDA ZA JUU KUSINI KUPATA VYENZO ZA KISASA ZA KILIMO KWA NJIA YA MKOPO WA AGRA NA ACT


Kati ya Nchi 22 za Afrika Tanzania imepata faida baada ya kupata ufadhili wa kupata Elimu ya Kilimo Hifadhi  Kutoka AGRA [Nyota ya kijani ]na kuwafanya Wakulima kuongeza kipato  cha mavuno kutoka gunia 4 hadi Gunia 28 kwa Ekari.
         Katibu Mtendaji Mkuu kutoka ACT Saidi  Mkomwa amesema jumla ya wakulima 100,000 kutoka  Bara la Afrika wamepata Elimu ya Kilimo Hifadhi jambo lililosababisha ongezeko la mavuno na kuifanya AGRA kuwajibika kutafuta masoko kwa mazao yanayozalishwa Afrika.


Afisa Mtendaji wa Kilimo Hifadhi kutoka Kenya Saidi Mkomwa amesema juhudi zinazofanywa hivi sasa na ATC ni kuhakikisha wakulima waliopewa Elimu ya Kilimo Hifadhi wanakuwa walimu kwa wakulima wenzao ili kasi ya uzalisha na kuondoa umasikini miongoni mwawananchi uwe mkubwa.


Katibu Mtendaji Mkuu wa Shirika la ACT  Kutoka Kenya Saidi Mkomwa amesema hayo wakati wa mafunzo kwa wakulima 50 kutoka mikoa ya Ruvuma,Iringa na Njombe amesema  Bara la Afrika lina utajiri mkubwa wa Ardhi kwani nao wawekezaji wa Kilimo wanajivunia  Hekta 1,000,000 za Ardhi za Kilimo Hifadhi, hivyo vijana hawana haja ya kukimbilia Ulaya wakiuacha utajiri Nchini mwao.

 Wakulima kutoka nyanda za juu kusi wakiwa katika mjadala mkoani Njombe katika ukumbi wa fm

Katika Nchi 22 za Bara la Afrika zinazo fadhiliwa na AGRA, katika Kilimo Hifadhi  kazi kubwa iliyo baki  ni kuwakopesha wakulima vifaa vya kisasa, pamoja na kuwaunganisha na Taasisi za fedha  ili  waweze kupata mikopo.alimaliza katibu saidi Mkomwa

 Wakulima wakiwa katika majaribio kuzijua dawa mbalimbali za kilimo huku wakisikiliza kwa makini matumizi halisi ya Pembejeo

Mtaalamu wa Kilimo Kanda ya Kusini Abiudi Gamba amesema anajivunia Elimu ya Kilimo Hifadhi kwa kuwa Wakulima kutoka wilaya za Ludewa, njombe, Songea Vijijini na Namtumbo  wamekuwa wataalamu katika Kilimo, Naye Mkulima Kutoka Kijiji cha Namatuhi Songea Vijijini Winiley Nindi amesema kutokana na utaalamu alioupata katika Mafunzo ya siku nne kutoka ACT  utamwezesha kuongeza mapato zaidi.Katika Nchi 22 za Bara la Afrika zinazo fadhiliwa na AGRA, katika Kilimo Hifadhi  kazi kubwa iliyo baki  ni kuwakopesha wakulima vifaa vya kisasa, pamoja na kuwaunganisha na Taasisi za fedha  ili  waweze kupata mikopo.alimaliza katibu saidi Mkomwa

No comments:

Post a Comment