KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, August 9, 2016

WANANCHI WA MKOA WA RUVUMA WANEEMEKA NA ONGEZEKO LA SOKO LA BIASHARA YA MAZAO YA NAFAKA BAADA MASISTA WA SHIRIKA LA MTAKATIFU AGNESS CHIPOLE KUFUNGUA KIWANDA CHA KUSINDIKA SEMBE CHENYE UWEZO WA KUSINDIKA TANI 50 ZA MAHINDI KWA SIKU

 Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Arusha Mh. Askofu Josphat Lebulu aesea maana halisi ya Utaw ni kujitoa kwa ajili ya wengine na siyo kwa maslahi ya shirika tu. Hivo amewaambia Masisita Kitendo cha kuanzisha mradi wa kusindika Sembe ni utume uliotukuka kwa jamii inayowazunguka. Uzinduzi wa Kiwanda cha Sembe cha Masista wa Mt Agness Chipole umeenda sambamba na Maadhimisho ya Jubilei ya mika 75 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo.
 Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Arusha Mh. Askofu Josphat Lebulu akijiandaa tayari kwa kubariki kiwanda amewapongeza Mmasista kwa kuibua mradi ambao utapunguza hadha ya kutafuta masoko ya mazao.

Kiwanda cha Masista wa Chipole kwa sasa kinafungasha unga katika Ujazo wa mifuko ya Kilogramu 5, kilogramu 10 na kilo 25. Pia wananchi huleta mahindi yao kiwandani na kuuza kwa bei ya Serikali.

Mradi wa Kiwanda cha kusindika Nafaka cha Chipole  kina uwezo wa kusaga Tani 1500 kwa mwezi jambo litakalosaidia kuondoa changamoto ya Soko la Mahindi Mkoani Ruvuma


Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha kusindika Mahindi cha chipole Altemius  Millinga amesema kutokana na Mradi wa Umeme wa Tulila Chipole kutoa Umeme mwingi  imebidi kuongeza Mradi ambao utainua  uchumi cha wananchi wa vijiji vinavyozunguka eneo la Mradi kwa kuweka kiwanda cha kusindika unga wa mahindi

Masista wa Mtakatifu Agness wa Chipole wamesema Shirika lao kila wakati linatafuta njia za kuongeza Fursa kwa wananchi wa vijiji vinavyozunguka Shirika hilo  ilik kuwaondolea changamoto ya kukosa Masoko ya Mazao wanayozalisha katika kudumisha ujiani mwema na udugu. Pichani ni Mama Mkubwa wa Shirika Sr. Maria Florida Chingu (OSB)
 Askofu Mkuu wa jimbo Katoliki la Arusha Mhashamu Askofu Josphat Lebulu aliyekuwa mgeni Rasmi katika Jubilei ya Miaka 75 ya kuanzishwa kwa shirika la Masista wa Chipole akibariki na kuzindua Kiwanda cha Sembe cha Masista wa Chipole Songea Vijijini.Mhashamu Askofu  Mkuu wa Jimbo Kaoliki la Arusha Askofu Josphat Lebulu  amewapongeza watawa  wa Kike Masista wa Mtakatifu Agness Chipole  kwa kubuni Mradi wa Usndikaji wa Nafaka za Mahindi kwa kuweka kiwanda chenye uwezo wa kusindika Tani 50 za Unga wa Sembe kwa siku.


Ghala la kjisasa ambalo lime jengwa katika kiwanda cha kusindika unga katika shilika la watawa wa Mtakatifu Agines Chipole
                        Haya ni mantank ya kuhifadhi mahindi kabla la kuanza kukobolewa
                        Haya ni maghala ya dharura ambayo yalijengwa wakati wa ujenzi wa kiwanda


                         Ghala jipya ambalo lime jengwa kwa ajili ya kuweka unga ulio sagwa
                                                                 Ghala likionekana kwa upande mbelekiwanda cha kusaga nafaka kinavyo onekana kwa mbali

Mradi wa Kiwanda cha kusindika Nafaka cha Chipole  kina uwezo wa kusaga Tani 1500 kwa mwezi jambo litgakalosaidia kuondoa changamoto ya Soko la Mahindi Mkoa wa Ruvuma, mkoa wa Ruvuma huzalisha tani milioni 1.4 na shilika la hifadhi la chakula mwaka jana lilinunua tani 15 ,000 na mahindi yanayo babi mkulima hulazimika kutafuta soko  na kuuza mahindi kwa hasara ya kilo kwa shilingi 150
                    Huu nimwonekano wa kiwanda cha kusaga unga katika eneo la chipole Songea Vijijini
             Mashine ya kusaga unga ina vipere vingi hadi unga unapo toka hicho ni kinu cha kusagia
             Mashine ya kusaga unga ina vipere vingi hadi unga unapo toka hicho ni kinu cha kusagia
             Mashine ya kusaga unga ina vipere vingi hadi unga unapo toka hicho ni kinu cha kusagia
                             Mashine ya ya kusaga unga ambayo ina jiendesha ki Automatic
              kinu cha mashine cha kupokea mahindi yaliyo kobolewa tayari kwa kupelekwa juu ili ya sagwe


Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha Josphat Lebulu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kiwanda cha kusindika Sembe, amesema kazi ya Kanisa ni kubuni Miradi ambayo inawanufaisha wananchi walio karibu na shirika la masista wa Chipole . Mradi wa Usindikaji utaweza kuongeza Soko la Mahindi kwa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.

                             Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha Josphat Lebulu
Mhashamu Askofu mkuu wa jimbo la Arusha Josphat Lebulu akiwasifu watawa wa Mtakatifu ASgines Chipole kwa kuweza kusogeza huduma mhimu ya upatikanaji wa kiwanda cha kusaga unga
                                  Masista wa mtakatifu Agnes Chipole wakifurahia ufunguzi wa kiwanda hicho
Mhashamu Askofu mkuu wa jimbo la Arusha Josphat Lebulu akikagua kiwanda cha kusaga unga Chipole
Mwenyekiti wa Bodi ya kiwanda cha kusaga unga Altemius  Millinga akibadilisha mawazo na Mama mkubwa wa Chipole
Mwenyekiti wa Bodi ya kiwanda cAltemius  Millingaha kusindika unga Altemius  Millinga akipeana mawazo ya kuongeza kiwanda kingine cha Mbinga ambacho kita kuwa na uwezo wa kusaga tani 100 kwa siku

No comments:

Post a Comment