KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, August 3, 2016

MKUU WA MKOA WA RUVUMA BINILITH MAHENGE AFANYA ZIARA YA GHAFULA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA RUVUMA


MKUU WA MKOA WA RUVUMA AMEFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA RUVUMA NA KUBAINI CHANGAMOTO MBALIMBALI IKIWEMO UKOSEFU VIFAA TIBA IKIWEMO GLOVES, NYUZI NA DAWA ZA KUTULIZA MAUMIVU.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge ameutaka Uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma  kuwajengea Jiko wauguzi wa Nje na kutatua Changamoto  ya ukosefu wa nyuzi za kushunea kwenye upasuaji.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge ameyasema hayo katika ziara ya kushitukiza katika Hospitali ya Mkoa na kukuta kuna choo kimoja tu kinachotumiwa na watu wasiopungua 250 .


Wauguzi wa wagonjwa wameulalamikia Uongozi wa Hospitali ya Rufaa kwa kukosa vitu vidogovidogo na kuwalazimu kwenda kununua nje, pamoja na kukosa sehemu ya kupikia, wamesema kwa sasa wanapikia nje.

wauguzi kutoka maeneo mbalimbali katika mkoa wa ruvuma

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr. Binilith Satano Mahenge amesema changamoto ndogo ndogo za kukosa vyoo, ukosefu wa Gloves na nyuzi katika hospitali kunaweza kuifanya Serikali iliyopo Madarakani ikashindwa  kuaminika na wananchi Ni juu ya Uongozi wa Hospitali kufanya Ziara katika vitengo mbalimbali kubaini changamoto  za Hospitali.


Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma Dr Philis Nyimbi amesema ukosefu wa Vifaa katika Hospitali hiyo inatokana na msongamano wa wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali


Katika  Ziara hiyo ya kushtukiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma  Dr. Mahenge amebaini ukosefu wa sehemu  ya kupikia, ukosefu wa dawa za Maumivu na uharibifu wa Mashine za Utra Saund ambazo mpaka sasa  zinatimiza miaka 2 bila kutengenezwa.  

 Mkuu wa Mkoa Dr Binilith Satano Mahenga akitoa agizo la kuwa jengea banda la kupikia kwa wauguzi wa nje
 Msafara wa waganga wakiwa katika ziara ya kusutukiza ya mkuu wa mkoa ambayo ziara hiyo ili baini changamoto za kuto kuwa na vyoo.dawa za m,aumivu na baadhi ya Mashine kuharibika
 Wafanyakazi wa Hospitali wakisikiliza kwa makini maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuhusu jinsi ya kuweza kutatua matatizo ya Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Damas Kayera akipokea Maagizo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge juu ya ujenzi wa vyoo vya wauguzi wa nje pamoja na kujenga banda la kupikia
katibu wa hospitali akieleza kuhusu damu ya akiba katika hosipatali ya Mkoa wa Ruvuma na kusema damu ya akiba iliyopo ni yuniti kumi tu ukilinganisha na mahitaji yanayo takiwa Hospitali ya Mkoa kwa siku hutumia yuniti kumi za Damu

No comments:

Post a Comment