KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, May 18, 2017

JESHI LA POLISI MKOA WA RUVUMA KWA KUSHIRIKIANA NA AFISA TARAFA WA TARAFA YA MUHUKURU SALMA MAPUNDA WAENDELEA NA MAPAMBANO DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA KWA KUTEKETEZA MASHAMBA YA BANGI


Afisa tarafa wa Tarafa ya Muhukuru Salma Mapunda akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Songea katika zoezi la kuteketeza bangi iliyooteshwa shambani amesema shamba lenye ukubwa wa ekari 2 linaloteketezwa lilibainika baada ya wananchi wenye kuchukia biashara ya Madawa ya kulevya kwa kushirikiana na Serikali ya Kijiji kutoa taarifa za uwepo wa shamba hilo.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limefanikiwa kuteketeza Shamba hilo la Bangi lenye ukubwa wa ekari 2 katika Kijiji cha Manyamba Kata ya Muhukulu barabarani Songea Vijijini.

 Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa imara katika mapambano dhidi ya Vita hii ya Madawa ya Kulevya ambayo ni tishio kwa Vijana.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Manyamba akishiriki katika zoezi la kuteketeza Bangi amesema yeye kama kiongozi wa Serikali ataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na Viongozi wengine katika Mapambano dhidi ya Zao la Bangi amesema tatizo lililopo wakulima wa bangi wanahamia kinyemela katika vijiji kwa kutafuta maeneo mazuri ya kulima wanapopata wanaamua kulima Bangi badala ya kulima mazao ya chakula
 Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Manyamba anasema, inakuwa vigumu kuyabaini mashamba hayo wanapoanza kilimo kwa kuwa hawaripoti katika Uongozi wa Vijiji husika wao huchukua maeneo kupitia kufuata wenzao na baadaye inabainika bangi ikiwa imeoteshwa na pengine imeshakuwa kupitia doria za msako wa mashamba yanayolimwa bangi hizo.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Manyamba anasema vijana watambue kuendelea kulima Bangi hawatakuwa salama kwa kuwa Serikali ina mkono mrefu badala yake wanaweza kulima Maharege, Ufuta na mahindi mazao ambayo wakilima hawana shida ya kukimbizana na Serikali.
 Mwanasheria wa Serikali akiwa katika Oparesheni hiyo ya Kuteketeza Bangi katika shamba lililopo Msitu wa Kijiji cha Manyamba Muhukuru Songea Vijijini amesema sheria ya sasa hivi iko wazi na endapo mtuhumiwa anabainika na vielelezo vikitimia adhabu yake haina mbadala hivyo ni vyema wananchi wakaacha kabisa kujishughulisha na kilimo cha bangi badala yake watafute kazi zingine.
 Mwanasheria wa Serikali akishiriki zoezi la kufyeka Bangi iliyokuwa imeoteshwa katika Shamba hilo Kijiji cha Manyamba Tarafa ya Muhukuru.

Afisa tarafa wa Tarafa ya Muhukuru amesema wananchi kutokana na kuzungukwa na Hifadhi za Misitu minene za wanyama na milima mikali ndiyo sababu hutumia kulima bangi wakijua hakuna mtu anayeweza kutambua uwepo wa mashamba hayo.

 Kazi ya uteketezaji wa zao la Bangi ikiendelea ikiongozwa na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Muhukuru Salma Mapunda akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema kwa kushirikiana na Vijana wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Songea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma ACP Zuberi Mwombeji amesema kampeni ya kuteketeza madawa ya kulevya inaendelea Mwananchi yeyote mwenye Taarifa za kuwepo kwa mashamba ya Bangi au taarifa za uwepo wa Biashara ya Madawa ya Kulevya atoe taarifa Jeshi la Polisi.


Mpaka sasa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limeshafanikiwa kuteketeza  Mashamba ya Bangi Ekari 34

Namna Kilimo cha bangi kinavyohudumiwa kwa umakini hapo shamba lenye ukubwa wa Ekari mbili likiwa limeoteswa bangi pekee pasipo kuchanganya zao lolote. Wakulima wa kilimo hiki sasa wamebuni mbinu ya kulima maeneo ya mbali yenye milima na misitu mizito wakiamini si rahisi vyombo vya dola kuyafikia maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment