KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, May 23, 2017

WANANCHI WA WILAYA YA NYASA WANUFAIKA NA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA KISASA CHINI YA USIMAMIZI NA UFUATILIAJI WA MBUNGE WA JIMBO LA NYASA NAIBU WAZIRI WA ELIMU MHANDISI STELLA MANNYANYA

 Mhandisi Stella Manyanya akielekea akishuka katika Ndege ya ATCL kwenye uwanja wa Ndege wa Songea tayari kuelekea wilayani Nyasa kwa ajili ya kukabidhi vifaa tiba.
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi akikabidhi Vifaa tiba vikiwemoVitanda vya kujifungulia akina Mama, Xray Mashine, Utra Sound, Will chair, Magodoro, Vitanda vya Wodi ya wazazi na vingine  katika Kituo cha Afya cha Mbamba Bay wilayani Nyasa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji amesema ameshirikiana na viongozi wa Halmashauri ya wilaya kupigania kupatikana kwa vifaa hivyo ili kukabiliana na vifo vya Mama na Mtoto wakati wa Uzazi.
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi amesema kupatikana kwa Vifaa vilivyokabidhiwa kumetokana na ushirikiano uliopo kati ya Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa wakiwemo Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Dr Osca Albano Mbyuzi,  jambo ambalo linasaidia katika kuwahudumia wananchi wa Wilaya yaNyasa ambao walikuwa wakiifuata huduma hiyo umbali mrefu kwa kutumia usafiri usio salama kama wa Pikipiki na kuhatarisha maisha ya mzazi.
 Wananchi waliohudhuria katika kukabidhi vifaa hivyo wameishukuru Serikali na mbunge wa Jimbo la Nyasa kwa kuwapunguzia adha waliyokuwa wakiipata kwa kufuata huduma za upasuaji na uzazi salama, wamesema awali walikuwa wakitumia kiasi kikubwa cha nauli kuvifikia vituo vyenye huduma bora za Afya ya uzazi jambo ambalo lilikuwa likihatarisha maisha ya wazazi.
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya akikabidhi vifaa hivyo ameomba wataalamu kuvigawa kadiri ya mahitaji kwa kuvisambaza katika vituo mbalimbali ili kuwapunguzia umbali wa kutembea kufuata huduma za dharula hasa kwa wazazi.
 Aidha Kaimu Mkuu wa wilaya ya Nyasa ambaye ni Mkuu wa wilaya ya tunduru Juma Homera akipokea Vifaa hivyo amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Nyasa na kuwaomba wananchi na wataalamu wa afya kuvitunza vifaa hivyo kadiri ya uthamani wake, amesema si rahisi Kituo cha Afya kikawa na Vifaa vyenye tija kwa wingi huo hivyo wana wajibu wa kuthamini mchango wa wadau waliwezesha kupatikana vifaa hivyo kwa kuvilinda visiharibike au kupotea.
 Kaimu Mkuu wa wilaya ya Nyasa amesema jambo lililofanywa na Naibu Waziri wa Elimu linastahili kuigwa kwa kuwa wapo wabunge ambao wamekuwa wakitelekeza Majimbo yao wapo wananchi wanatamani kupata Vifaa kama hivi kwa ustawi wa wananchi kwa kuwa Afya ndio msingi wa kila jambo.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Mbamba Bay Dr Aaron Hyera ameshukuru kwa kupata Vifaa tiba ambazo vitasaidia kusovu baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zikiikabili Halmashauri ya wilaya ya Nyasa.
 Akizitaja baadhi ya Changamoto wanazokabiliana nazo katika utoaji wa Huduma za Afya ni pamoja na uhaba maghari kutokana na uchakavu wa baadhi ya Magari ya wagonjwa (Ambulece), upatikanaji mdogo wa fedha za ruzuku za kuwezesha kununua vifaa tiba kadiri ya Bajeti wanazozipitisha, uhaba wa watumishi hususani waganga na wauguzi ambapo kwa sasa kuna upungufu wa watumishi 180 waliopo ni 228 katika vituo vya kutolea huduma za afya, wana Medical Officer mmoja tu na mwingine wanatarajia kumpokea hivi karibuni.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Mbamba Bay amesema changamoto nyingine ni upungufu wa Dawa kutoka MSd ambapo kati ya Bajeti wanayoomba ya madawa upatikanaji wa dawa zinazokuja ni 50% tu au chini ya hapo jambo ambalo linawawia vigumu namna ya kuzigawa katika vituo kadiri ya Mahitaji.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Mbamba Bay Dr. Aaron hyera amesema upatikanaji wa Vifaa hivi vitasaidia sana kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ambapo amesema kwa sasa takwimu za vifo vitokanavyo na uzazi vimepungua kutokana na elimu ya kuwataka wazazi kuhudhuria kliniki ambapo mwaka 2014 kati ya wanawake laki moja wanaojifungua kulikuwa na vifo 78 vitokanavyo na uzazi ambavyo vimepungua hadi kufikia vifo 23 katika wazazi laki moja kwa mwaka 2016.
 Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mbamba Bay Dr Paulo Matinde na wauguzi wa Kituo cha Mbamba Bay wamepongeza jitihada zilizofanyika na kufanikisha kukamilika kwa ujenzi wa Jengo la Upasuaji na Wodi ya wazazi pamoja na upatikanaji wa Vifaa tiba utaongeza hari ya ufanyaji kazi kwa kuwa vitendea kazi vimeongezeka ambapo kituo kilikuwa hakina mashine ya utrasound na xray na vitanda vya kujifungulia lakini sasa vyote vimepatikana wanachoomba wazazi kuja kujifungulia katika vituo vya Afya.
 Kaimu Mkuu wa wilaya ya Nyasa anasema kufanikisha kwa upatikanaji na utoaji wa huduma za Afya kunadhihirisha kauli ya Uchungu wa Mwana aujua Mzazi kwa kugusa maendeleo ya wazazi katika kuboresha afya ya mama na mtoto kwa wananchi wa wilaya ya Nyasa.
Wilaya ya Nyasa ina Vituo vya kutolea Huduma za Afya 35 ambapo kati ya hivyo vituo vya Afya  vinne vinamilikiwa na serikali pamoja na Zahanati 21 za Serikali, vingine ni vya Mashirika ya Dini na Binafsi. Kwa sasa haina Hospitali ya wilaya jitihada zinafanyika za kupata eneo la kutosha kuwezesha Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.

No comments:

Post a Comment