KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, May 16, 2017

MAFUNZO YA UDEREVA YAPUNGUZA AJALI KWA ASILIMIA 60% SONGEA MKOANI RUVUMA


Vijana waendesha Boda boda Manispaa ya Songea wameiomba Serikali kuendesha Mafunzo ya Udereva wa Pikipiki na Magari Vijijini badala ya kuendesha Mafunzo hayo katika Vyuo vya Veta.


Vijana wapatao 238  waliomba Ombi hilo wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Madereva wa Bodaboda katika Vijiji vya Matimila na Mwenge Mshindo.

Vijana hao wamesema Ajali nyingi zilikuwa zinatokea kwa Vijana kutojua sheria za Usalama Barabarani, wapo vijana waliopoteza Maisha kwa kuwakimbia Askari wa Usalama Barabarani, wengine kutokana na mwendo kasi  na wengine kutokujua kusoma Alama za Barabarani

Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Ruvuma Abell Swai amewataka waliohitimu Mafunzo ya Udereva kuwa Makini kwa kufuata Sheria za Usalama Barabarani.
 Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Ruvuma Abell Swai amesema Mafunzo ya Udereva  wa  Pikipiki na Magari katika Mkoa wa Ruvuma umeweza kupunguza Ajali kwa asilimia 60% baada ya Madereva kutumia Alama za Barabarani na kuendesha kwa Mwendo wa Pole

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) Songea Gideon Ole Lairambe amewaomba Vijana na Wazee wanaotaka kuingia katika Fani ya Udereva waepukane na watu wanaowaahidi kuwapa leseni,  kwa sababu Leseni inatolewa kwa Madaraja yote baada ya Mtu kupitia Chuo cha Veta,
Amesema wapo Madereva waliopoteza Ajira kwa kuwa na Leseni Feki hivyo kila anayetaka kupata Leseni iliyo safi ajiunge ajiunge na Vyuo vya Ufundi VETA ambavyo kwa sasa vinatoa Mafunzo hata Vijijini.

 Vijana waliohitimu Mafunzo ya Udereva wakiwa katika Kata ya Mwenge Mwenge Mshindo wakisikiliza mafunzo kwa makini.
WAZEE  wakiongozwa na  Daudi Komba   wamesema  wanaomba mafunzo ya udereva wa fani zote utolewe zaidi vijijini ili vijana wapate elimu zaidi, amesma katika misako ya pikipiki itumike busara zaidi kuliko kutumia nguvu

No comments:

Post a Comment