KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, February 8, 2013

MILA NA DESTURI ZA MWAFRIKA KWA NINI HAZI FUATWI VILIVYO


 GOGO LA MAAJABU AMBALO VIONGOZI MBALIMBALI WALIKAA JUUYA GOGO HILO WALIFANIKIWA    KATIKA MAPAMBANO YA VITA VYA UKOMBOZI

Ndugu Msomaji wa Blog ya Songea Habari.blogspot.com. Napenda kukukaribisha ili uweze kuona Kitu kinachoitwa Imani kina maana gani.

Jambo la Msingi napenda kukurudisha katika Mila na Desturi ambazo zilikuwa zikiwafaa Wabantu. Ukumbuke kuwa Mila na Desturi za wenzetu hawa watu weupe au Wazungu ndio waliotuteka katika mila zao, huyu tunayemwita Mungu ambaye yupo katika Biblia na katika Kurani Tukufu .

Lakini hiyo haifanyi kuwa sisi Wabantu tulikuwa hatuna Mungu wetu. Hebu rudisha Mawazo yako nyuma, Jee hawa watu weupe tunaowaita Wazungu walikuwa wakijua lugha zetu la, 

Sasa hebu uone mimi Mungu wangu kwa Lugha yangu Mungu nilikuwa namwita Chapanga, wengine Nguluwi, Mulungu, Mnungu, Mluku .  hayo yote ni majina ya kibantu  yaliyo kuwa ya kitumika kumwita Mungu  hii ni kuthibitisha kuwa Waafrika walikuwa na Dini zao za Asili.

Kitu ambacho nataka kukuambia. katika kudai Uhuru Nchi mbalimbali za Africa zilikuwa na mila ya kutambika ili kupata Mafanikio, katika kuomba Mvua , kushinda Vita au Jambo lolote ambaloni Gumu.

Sasa hebu tuone Mfano mdogo katika Nchiya Msumbiji wakati wa Vita vya Frelimo na Wareno, Mkutano wa pili wa Vita hivyo ulifanyika Macheja mpakani na Tarafa ya Mhukuru Nchini Tanzania ,kitu cha ajabu wa kuu wote waliokuwa wakipigania Uhuru walikuwa hawa kai kwenye viti bali wali Tumia Gogo kubwa kukalia wakiwa na imani na gogo hilo kwa kupata ushindi .

Sasa tuingie Nchini Msumbiji tuone wenzetu walivyokuwa na Imani na gogo kubwa ambalo linasadikiwa Viongozi wote wa Afrika wameweza kukaa juu ya gogo hilo na kila aliyekaa hapo alifanikiwa kupata Ushindi.

Ziangalie kwa makini hizo picha hizo uone viongozi walivyokuwa wazalendo kwa kuipenda Nchi yao na mila zao.
 Mke wa Marehemu Moses Machel wakati wa mapambano wa vita vya msumbiji picha hiyo ili pigwa macheje Nchini Mozambiki
 Marehemu Samora Machel akipanga mashambulizi dhidi ya Wreno Nchini Mozambiq wakati ule
 Marehemu Candido Mondlane akiwa uwanja wa mipango ya vita Macheje Nchini Mozambiq
 Njia ya mapambano dhidi ya warenoili tegemea zaidi mto Ruvuma kwa uvushaji wa Silaha
 viongozi wandamizi wa Mozambiq aliye vaa kofia Samora Machel na wa mwisho ni Rais wa sasa wa msumbiji Armando Emillo Guebuza wakiwa wamekaka katitka Gogo la ukombozi
 Marehemu Samora Machel akitoa maagizo kwa ArmandoEmillo Geubuza wakiwa wamekalia gogo la ukombozi

No comments:

Post a Comment