KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, February 27, 2013

MKOA WA RUVUMA WAWAKUMBUKA MASHUJAA WALIO KUFA KWA KUNYONGWA WAKATI WA VITA VYA MAJIMAJI MWAKA 1906

Waziri wa Maliasili na Utalii Nchini Tanzania Balozi Hamis Kagasheki ameweza kuongoza Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya Majimaji walionyonga tar 27/02/1906 na Wajerumani ambapo Mashujaa 61 walizikwa katika Kaburi moja.
  1. Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma hukumbuka Mateso waliyoyapata Babu zao, Hapo wapo katika Viwanja vya Mashujaa Mahenge Manispaa ya Songea kushuhudia Maombolezo yaliyoongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamis Kagasheki. 
Uwanja wa Mashujaa Mahenge umezungukwa na picha za Mashujaa wa Vita vya Majimaji hiyo ni picha ya shujaa Chifu Songea Mbano
Hapo Mh. Balozi Hamis Kagasheki akiongoza Maandamano yaliyoanzia Sehemu waliyonyongwa hadi katika Uwanja wa Mashujaa

  1. Katika Maombolezo yaliyofanywa Viwanja vya Mashujaa Mahenge Mgeni Rasmi Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamis Kagasheki aliweza kuweka Ngao na Mkuki katika Mnara wa Mashujaa wa Vita vya Majimaji, hapo anaonekana akiweka Ngao.
  1. Waziri wa Maliasili Balozi Hamis Kagasheki akienda kuweka Ngao na Mkuki katika Mnara wa Mahujaa Mahenge.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu akiweka kinjenje
 Mkuu wa mkoa akirudi jukwaani baada ya kuweka silaha ya jadi aina ya kinjenje
 Bregedia akiwa katika mnara wa Mashujaa Mahenge akiweka Upinde na Mshale
  1.  Chifu wa Wangoni Mbano akiwakilisha Wangoni kwa kuweka Kinjenje na Rungu (Kibonga)  katika Mnara wa Mashujaa
  1. Katika kuwakumbuka Mashujaa waliotangulia mbele za Haki Jeshi la Wananchi limeweka Utaratibu Maalumu ikiwa ni pamoja na kulipua mizinga na Fataki katika kuwakenzi Mashujaa.
 Hapo wanajeshi wakiendelea kutoasalamuza maombelezikwa njia ya kijeshi
 Hiyo yote ninjia ya kuwakumbuka Mashujaa walio  Tangulia
 Ukiwa umepitia mafunzo ya kijeshi  utajua uchungu wanao upata waombolezaji hawa
 Nimoja ya kuomboleza kuinamisha kichwa chini ni dalili ya kumwomba mwenyezi Mungu awaweke Mahali pema Mashujaa  walioo tangulia Mbele zahaki


 Jeshi  unatakiwa kungangamala ,hebu ona jinsi mashujaa wanavyo omboleza katika kuwa kumbuka Mashujaa waliotangulia
 Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wakiwa katika viwanja vya mashujaa Mahenge Manispaa ya Songea
Jeshi la Wananchi wa Tanzania likitoka nje ya Uwanja wa Mashujaa baada ya
             kumaliza taratibu zote za Maombolezo kwa kuwakumbuka Mashujaa 61
             walionyongwa na kuzikwa katika kaburi moja

 Mwalimu Kaisi Ally kutoka dhehebu la Ahamadiya Mkoa wa Ruvuma akiwaombea mashujaa walio Tangulia wakati wa maombolezo  katika uwanja wa mashujaa manispaa ya songea
Mkuu wa Wilaya ya Rudewa Juma Madaha akiwa mmoja wa waombolezaji wa
           Mashujaa wa Vita vya Majimaji.
Wanajeshi wakilipua Mizinga kuashiria kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya Majimaji.
Wanajeshi wakilipua Mizinga kuashiria kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya Majimaji.
Wanajeshi wakilipua Mizinga kuashiria kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya Majimaji.

No comments:

Post a Comment