KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, June 21, 2014

KWA NINI WATU HAWAACHI VITENDO VYA USHIRIKINA ,WAONE WACHAWI WA SONGEA MKOANI RUVUMA


Ukishangaa ya Mussa uta Shangaa na ya Filauni ndivyo wasemavyo wa  Swahili . Ndugu yangu mara nyingine na panda kuongelea swala la ushirikina, kama hayajakukuta huwezi kuamini maswala ya Ushirikina.

Mimi mwandishi wa Habari hizi niko mkoani Ruvuma eneo ambalo una ambiwa kulifanyika vita vya majimaji, vita hivi vilikuwa na maana kwa kuwa risasi za mjerumani zili geuka kuwa maji na kushindwa kuwa zuru wangoni,Hata songea alipo taka kunyongwa kamba ili katika mara kadha kama si wasaliti Songea asinge kufa.

Hebu ni achane na hilo wazee wawili kutoka Parango ,mtaa wa Nandutu amekamatwa uchawi baada ya kubainika kuua wajukuu wake wane akidai ili kuwa ni mchezo wa kichawi. Mwingine ni MzeeAlex Haule ambaye naye ameua watoto wa Nne mwenyeji wa Kijiji cha Mshindo Luhila kati Mkoani Ruvuma,

Mzee Alex Haule yeye kasema alikuwa akiua watoto wake kila sikukuu akiona huruma kwa Mtoto wake alikuwa akialikia Mtu mwingine atekeleze tendo la kuua.Ndugu zangu hii siyo hadithi bali ni ukweli ulio wazi ukifika Eneo la Luhila katika Manispaa ya Songea ni kilometa tano kutoka Mjini nji iendayo Tunduru

Ukifika luhila Sheli chepuka mkono wa kulia ni mwendo wa nusu saa kutoka barabara ya Lami uta kuta kambi hapo,Sasa hebu nikuonyeshe picha za Washirikina walio kiri mbele ya Mganga Bint Ndembo kiboko cha Wachawi Ruvuma
Umati wawatu ukielekea Uwanja wa Zambi kuona Washirikina wanavyo umbuka ni kilometa tano tu kutoka Songea Mjini ,Bendera hiyo nyekundu ni kuonyesha eneo unalo ingia ukiwa mchawi ujue ni hatari,
Umewahi kuona kibuyu kikizunguza basi ukipata nafasi ukikutana na Mzee Alex Haule atakueleza kwa kirefu, unakiona kibuyu hicho alicho kamata hapo hana ujanja wa kishirikina kila kitu ana sema mwenyewe
Mzee Alex Haule akiwa amekaa Uwanja wa Zambi na Mganga wa Jadi Binti ndembo akieleza jinsi alivyo ua Watoto wake wa NNE kwa njia ya Ushirikina aliye kulia ni Mzee mshirikina Beda Nchimbi liye vaa shati jeupe ,Hivyo vipara vina maana yake fika uwanja wa zambi uta jua maana ya upara
Mzee Beda Nchimbi kutoka Parango Peramiho Songea Vijijini aliye vaa Shati Jeupe amambaye ameua wajukuu wanne akiwa uwanja wa Zambi akitubu Matendo maovu aliyo yafanya kwa Jamii
Bint Ndembo akiwa na kioo cha ajabu ambacho huangalia matendo mabovu yanayo tendwa na washirikina
Washirikina wakivua viatu mara wanapo ingia uwanja wa Zambi tayari kwa kuumbuliwa Maovu yao
Ukiangalia kwa Makini hapo wanapo kaa hao watu kuna duara la rangi nyeupa kwa hapo chini ukikalia duara hilo basi wewe kama Mshirikina utaeleza kila kitu ulicho kuwa nacho hata dawa unazo tumia uta eleza :Unachezea Bint Ndembo wewe:
Kutoka kulia ni Mzee Alex Haule ambaye ameua watoto wake wa Nne kwa ajili ya Sikukuu mbalimbali. wa kwanza kushoto ni mzee Beda Nchimbi ambaye naye ameua wajukuu wake Nne kwa ajili ya Kitoweo kama alivyo dai mwenyewe,

1 comment: