KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, July 7, 2014

MWENGE WA UHURU WAZINDUA NYUMBA YA UHAMIAJI RUVUMA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Rachel Stephen Kassanda akihutubia wananchi mbele ya Jengo la Makazi la Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma mara baada ya kulizindua katika kata ya  Mahenge Manispaa ya Songea. Amesema wapo wananchi wa Mkoa wa  Ruvuma wanaoshirikiana na Wahamiaji Haramu kuwasafirisha na kuwahifadhi katika maeneo malumu  amewaomba Wananchi kutoa ushirikiano kwa Idara ya Uhamiaji ili kutokomeza vitendo hivyo.
Kiongozi Mbio za Mwenge kitaifa Racher Stephen Kassanda amesema wahamiaji walio wengi kutoka Eretria, Somalia hupitia Mipaka ya Mkoa wa Ruvuma.
Pichani anayehutubia ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2014, anayefuatia katikati ni Afisa uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza na wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti.
 Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika Picha ya pamoja na Mwenge wa Uhuru katika Jengo la Makaazi la Afisa Uhamiaji lililozinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Racher Stephen Kassanda. Pichani aliye katikati ya viongozi wa Mbio za Mwenge ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza.
Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Mbio za Mwenge mara baada ya kuzindua Jengo lao.

Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza akisoma Risala kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa amesema lengo la kujenga nyumba za makazi na kuzikarabati ni kuondoa changamoto zinazokabili wafanyakazi wa Uhamiaji wanapokuwa nje pia kuleta ufanis katika kazi.
Mwenge wa Uhuru 2014 ukiwa na Viongozi wa Msafara wa Mbio za Mwenge Mkoani Ruvuma katika eneo la Mradi wa Jengo la Makaazi la Uhamiaji Mahenge Manispaa ya Songea. Wenye sare za Kitenge ni kikundi cha Kwaya ya Namtumbo

Mwenge wa Uhuru  ukiwa Mkoani Ruvuma umeweza kuzindua Miradi mbalikmbali katika wilaya za  Nyasa, Mbinga na wilaya ya  Songea  ambapo miongoni mwa miradi iliyozinduliwa ni pamoja na kuzindua Jengo la Makaazi la Uhamiaji lililogharimu shilingi 434,100,170. Mwenge unaendelea na Mbio zake katika wilaya ya Namtumbo na Tunduru.

Kaimu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Shaban Shaban akiwa tayari kupokea Mwenge wa Uhuru katika eneo la Jengo la Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Zacharia Nachoa aliyeshika taarifa akiwa katika Msafara wa Mbio za Mwenge Manispaa ya Songea kushiriki katika Uzinduzi wa Miradi iliyokamilika katika Halmashauri yake
 Katika Utunzaji wa Mazingira Mkoa wa Ruvuma, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Racher Kassanda aliweza kupanda Mti wa mkungu akiashiria kushiriki katika utunzaji wa mazingira.
 Afisa Uhamiaji mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza Akipokea Mwenge wa Uhuru ikiwa ni ishara ya Uzalendo ya Nchi ya Tanzania.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza akiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa kushoto ni Bw Shaban Mtumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma
Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma lililozinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Lililogharimu kiasi cha Shilingi 434,100,170. Lililopo Mahenge Manispaa ya Songea.
 Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza akisoma Taarifa ya Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Makazi ya Afisa Uhamiaji kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma akiwa na Ma WP wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa ruvuma katika eneo lililofanyika uzinduzi wa Nyumba ya Makazi iliyozinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2014.
Pichani wa pili kutoka kulia Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza akiwa watumishi wa Idara hiyo muda Mfupi kabla ya Msafara wa Mbio za Mwenge kuwasili katika eneo la Jengo la Uhamiaji tayari kwa kuzindua.
Mwasibu wa Idara ya Uhamiaji aliyeshika Mwenge katika eneo la Jengo la Makaazi la Uhamiaji.
Watumishi wa Idara ya Uhamiaji wakiwa katika eneo la Jengo la Uhamiaji wakisubiri kwa hamu kushuhudia Uzinduzi wa Jengo la Idara ya Uhamiaji lililozinduliwa na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Racher Kassanda  July 2014

No comments:

Post a Comment