KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, July 23, 2014

SEREKARI IMEJISAHAU VIPI HADI KULETA HOFU KWA BINADAMU WASIO NA KOSA ?



Viungo mbali mbali vya binadamu vimekutwa katika eneo la kutupa taka la Bunju mjini Dar es Salaam katika mazingira ambayo haijafahamika mara moja kuwa viungo hivyo vimetoka wapi.
Kwa mjibu wa Afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema viungo hivyo vya binadamu vilivyokutwa ni miguu,vidole ambavyo vilikutwa vikiwa vimefungwa ndani ya mifuko.
Hata pamoja na viungo hivyo pia vifaa vya upasuaji vimekutwa zikiwemo glovuzi.
Mtu mmoja anashikiliwa kuhusishwa na tukio hilo ambaye ni dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo lililobeba viungo hivyo vya binadamu.
Haijafahamika mara moja miili hiyo ya binadamu imetolewa wapi na ilipelekwa eneo hilo kwa lengo gani.
Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikikabiliwa na tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino ambapo viungo vyao huchukuliwa,japo kuwa viungo hivi vilivyokutwa kwa sasa bado havihusishwi moja kwa moja na matukio ya mashambulizi na mauaji ya walemavu hao

IMG-20140721-WA0008


No comments:

Post a Comment