KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, July 30, 2014

WAISLAMU WATAKIWA KUWA NA UMOJA UTENGANO UNA LETA MADHARA IKWA PAMOJA NA VITA


Waislamu Mkoani Ruvuma wametakiwa kuwa na umoja na kufuata Mambo mazuri ambayo hayawezi kuiweka Nchi Mahali pabaya, Umoja Mshikamano na kuaminiana ndiyo silaha ya kuweza kuendeleza Amani.

Mataifa ya Waarabu yameingia katika Vita na kukosa Amani kutokana na Unafiki na kuyajali Mataifa makubwa. Hayo yamesemwa katika kusherehekea Sikukuu ya Iddi Fitri Mjini Songea.

Sheikh Shaban Chitete wa Masijidi Huda amesema endapo Waislamu watakuwa wanafiki basi huo ndio utakuwa mwanya wa watu wabaya kupata nafasi ya kuwagombanisha, amesema katika kuitafuta Katiba Mpya Wabunge tuliowachagua wamejigawa na kujiita Ukawa hiyo ni kutaka kufuja Fedha za Wananchi .

Waumini wa Dini ya kiislam Katika Misikiti mbalimbali ya Manispaa ya Songea wamemuomba Mungu aendekeze Amani na Utulivu tulionao na kuwaombea wale wenye nia ya kutaka Taifa la Tanzania liwe na Mfarakano washindwe. Alahamdulilahi Labiramina,

Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Ruvuma Mauridi Hassan Said ameiomba Serikali kuangalia upya kuhusu Ujenzi wa Mabucha ya Nguruwe, kuweka Mabucha ya Nguruwe hadharani kama ilivyo katika Soko la Mazao SODECO ni kuwadhalilisha Waislam. Waislamu wanashindwa kununua bidhaa katika Soko la SODECO kutokana na Mabucha ya Nguruwe kuwa wazi wazi.
Sheikh Shabani Chitete akiwa katika membali ya Masijid Huda Mabatini akitoa Hotuba ya Sikukuu ya Iddi Fitiri
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amewataka Waislamu kuwaimarisha watoto katika kujiendeleza kielimu

Katibu wa BAKWATA amesema katika kuendeleza Elimu kila Msikiti utakuwa na Shamba la zao la chakula, pia kila Msikiti utakuwa na Orodha ya Waislam na orodha zao kila msikiti uhakikishe una ekari mbili za miti ili kulinda mazingira.
Wanafunzi wa Shule ya wasichana Songea wakiwa nje ya Msikiti wa Masijidi Huda wakifurahia Iddi Fitiri
Mzee na Familia yake wakitoka kuswali katika msikiti wa Huda Mabatini Manspaa ya Songea
                                                                swala ya iddi firiri
Iddi Mbara kwa waislamu, wahimizwa kuwa na upendo wenyewe kwa wenyewe
waumini wa msikiti wa mjini kati wakiwa katika dua la kupombea amani Serekari ya Tanzania

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu ameyasema hayo katika Baraza la Iddi lililofanyika katika ukumbi wa Songea girls. Amesema Waislamu ili kuyafikia Maendeleo ya kweli ni lazima wajidhatiti katika Elimu hasa kwa kuwaendeleza watoto wao.

Masijidi Huda katika Manisipaa ya Songea waumini wakiwa ndani ya Msikiti
Hivyo hivyo wanaume walio kosa nafasi ndani ya Msikiti wakiwa wana swali nje ya Msikiti wa Mjini kati Songea
Akina mama katika Msikiti wa Mjini Kati katika Manispaa ya Songea wakiwa wametandika Mikeka Nje baada ya kukosa nafasi ndani ya Msikiti
                               wanawake wakiwa msikiti wa mjini kati songea
Akina mama walio miminika katika Msikiti wa Masijidi Huda wakiwa Tayari kwa Swala ya Iddi

Aidha Katibu wa BAKWATA Maurid Hassan Said amesema Waislamu walio wengi ni wakulima, mwaka huu kumekuwa na Mahindi mengi. Mwaka jana Serikali ilinunua Tani 53,000 tu za mahindi. Mwaka huu Inatarajia kununua Tani 48,000  Nipungufu kuliko mwaka jana katika ununuzi. Wameiomba Serikali kuongeza ununuzi ili kuwaokoa Wananchi katika kukabiliana na Umaskini.
Waisilamu Katika Manspaa ya Songea Wakiombea Amani wakati wa Swala ya Iddi
Waisilamu wakiwa katika swala ya iddi katika msikiti wa Huda Mabatini mjini Songea

No comments:

Post a Comment