KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, September 26, 2015

KUNING'INIZA MABANGO KWENYE NYAYA ZA UMEME NI HATARI KWA MAISHA SONGEA


Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Songea Rafaeli Malini ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari, amesema kwa sasa katika Manispaa ya Songea Vyama vya Kisiasa vimekuwa vikipachika Mabango kwenye Nyaya za Umeme, simu na Nyumba za watu ambapo kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.


Kampeni za Uchaguzi Mkoa wa Ruvuma zinaendelea kwa kishindo kila Chama kikiwa na uhakika wa kushinda Oktoba 25.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Rafaeli Malini amesema amejaribu kuwasiliana na Vyama vya Siasa kuwa aqmbia wanachama wao  kuacha kubandika Mabango bila idhini ya watu wanaomiliki katika maeneo hayo pia kuacha kuning’iniza mabango  katika nyaya za umeme

Mratibu wa CHADEMA Kanda ya Kusini Frank Mwaisumba amewaomba Viongozi wa Serikali za Mitaa mahali walipo kusimamia na kukemea kwa mtu yeyote atakayeonekana akibandika Mabango katika sehemu zisizohusika, Vijana wamewahimiza Vijana wenzao kuacha tabia ya kuhatarisha maisha yao kwa kuweka Mabango kwenye Nyaya za Umeme


Wananchi wa Manispaa ya Songea wametakiwa kuacha mambo ambayo yanaweza kuwafanya wapoteze maisha ikiwa ni pamoja na kupachika mabango kwenye nyaya za umeme.


Katibu wa Uwt Mkoa wa Ruvuma Chiku Mohamed Masanja amesema kuning`iniza Mabango na kuchana Mabango ya Vyama vya siasa ni kinyume cha Sheria.


Kaimu Meneja wa TANESCO Haruna Mwachula akiongea kwa njia ya simu amesema kutundika Mabango kwenye Nyaya za Umeme ni kulihujumu Shirika la TANESCO na kulikosesha mapato. Pia ni kuhatarisha Maisha kwa wanao tundika na wapiti njia.

No comments:

Post a Comment