KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, December 17, 2015

MABARAZA YA MADIWANI HALMASHAURI ZA WILAYA YA MADABA, NAMTUMBO NA MANISPAA YA SONGEA

 Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Ndirimalitembo Cerensesia Kapinga akitafakali majukumu yaliyo mbele yake ya kushirikiana na wananchi kuleta maendeleo katika kata yake ikiwemo na kupunguza vifo vya mama na mtoto, kutengeneza miundo mbinu ya Barbara kusogeza Zahanati kwa wananchi wake pamoja na kuleta mahusiano kati ya watendaji na wananchi
 Mh.Diwani Yobo na Mama Banana wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani Manspaa ya Songea
  Mh. Mussa  NdombaDiwani wa kata ya Shule ya Tanga kupitia CHADEMA akitafakari kazi iliyoko mbele yake ya kuhakikisha wananchi wa Kata yake wanapata maendeleo kwa kutatua kero zinazowakabili.
Mh,Diwani wa Kata ya Mjimwema Oddo Mbunda akiwa katika Baraza la Madiwani Manspaa ya Songea
 Mbunge wa jimbo la Madaba Joseph Kizito Mwagama akifurahia kuona Baraza la Madiwani limepatikana katika jimbo lake na kwamba ameongezewa timu ya kufanya nayo kazi katika kuhakikisha jimbo la Madaba linasonga mbele kwa maendeleo kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw. Robert Mageni. Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akisalimiana na wajumbe wa Baraza la Madaba.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akiwa katika Halmashauri ya Madaba
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba aliyechaguliwa kuongoza halmashauri mpya ya madaba ambayo imegawika kutoka halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini Mh. Mfikwa kulia akiwa na makamu Mwenyekiti wake katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba Robert Mageni na Mwenyekiti wa halmashauri ya Madaba Mfikwa wakiwa na viongozi wa Mkoa nje ya ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba.
 Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma katika kikao cha Baraza la Madiwani wilayani Namtumbo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akiwa Halimashauri ya Madaba Songea Vivijijni Akita Sahii kitabu cha Wageni
 Mkurugenzi  Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Ally Mpenye akiwashukuru wajumbe wa baraza la Madiwani kwa kumpa dhamana ya kuongoza halmashauri na kuomba ushirikiano kwa Madiwani katika kupigania maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya.Mkurugenzi Mtendaji wa Ally Mpenye  amemwomba mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuacha kuwa kingia kifua watu wanao kwepa kulipa kodi na kukimbilia kwake
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akisalimiana na Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo.Wakwanza Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Ally Mpenye Anaye Fuatia ni Mwenyekiti wa Halimashauri ya wilaya ya Namtumbo Dani Nyambo
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akibadilishana mawazo na viongozi wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo jinsi ya kusukuma maendeleo ya kasi katika halmashauri za wilaya kwa kutumia fursa zilizopo ndani ya halmashauri.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Dani Nyambo akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu katika ofisi za wilaya ya Namtumbo.
 Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Bakar Nalicho akifuatilia kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo.
 Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo wakiwa katika kikao cha uzinduzi wa Baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo. Katikati ni mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu
 Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu mara baada ya kikao cha kwanza cha kulizindua baraza hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu amesema pamoja na na kutii amuri ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mh John Pombe Maguli .Lakini maswala mengine inabidi tujiwekee utaratibu wenyewe  kama watu kukojoa ovyo hadharani ,kutupa makopo ya maji pamoja na karatasi za vyocha  amesema  mtu  yoyote atakaye kamatwa atatozwa faini ya shilingi 50,000/= au kwenda jela

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu amewataka madiwaku kufanya kazi walizo waahidi wana nchi waache kabisa kulifanya baraza la madiwani kuwa sehemu ya marumbano ya kisiasa.
 Mbunge wa Jimbo la Sonmgea Mjini Leonidas Gama akiwa na Viongozi wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Songea.
 Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Leonidas Gama akiwa katika Kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Songea ameahidi kushirikiana na madiwani katika kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Songea mjini.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Songea Mama Chilooko  aliyeibuka kidedea dhidi ya wagombea wenzake katika nafasi ya unaibu meya katika halmashauri ya Manispaa ya Songea
 Mh. Mussa Diwani wa kata ya Shule ya Tanga kupitia CHADEMA akitafakari kazi iliyoko mbele yake ya kuhakikisha wananchi wa Kata yake wanapata maendeleo kwa kutatua kero zinazowakabili.
 Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea wamejipanga kuwatumikia wananchi ili kuhakikisha kero za wananchi zinamalizwa kwa kushirikiana na watendaji wa halmashauri ya Manispaa ya Songea ambayo ndio makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma kwani tumaini la wananchi ni kuona halmashauri hiyo inakluwa mfano wa halmashauri zingine katika kupiga hatua kimaendeleo. wa kwanza kulima ni diwani wa viti maalum kata ya Matarawe Judith Mbogoro kupitia chama cha CCM

Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wamesema wana ungana na Rais Mteule Dr. John Pombe Magufuli katika kuijenga Nchi ki maendeleo na Uchumi.
Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wamemuomba Rais John Pombe Magufuli kuweka kipaumbele changamoto zinazo ukabili Mkoa wa Ruvuma kama Viwanda, Pembejeo za kilimo pamoja na kukuza Mitaji.
 watendaji katika Manispaa ya Songea wakifuatilia maazimio ya mwelekeo wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Songea katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo la Songea Mjini
 Mwandishi wa Habari wa CHANEL TEn Marietha Msembele akifutilia hoja la baraza la madiwani la manispaa ya songea. Hapo akiwa na tabasamu linaloashiria kuifurahia kazi yake
 Wataalamu na wakuu wa Idara mbalimbali katika Manispaa ya Songea wakifuatilia hoja katika kikao cha kwanza cha Baraza la madiwani Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Vijana nao wamesema Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr. John Pombe Magufuli alihaidi Mikopo kwa Vijana pia kuboresha Maisha ya Watanzania na ahadi zake amehaidi kwa kumtanguliza  Mwenyezi Mungu.
 Ni katika Ukumbi wa manispaa ya Songea Baraza la Madiwani likifanya kikao cha uzinduzi wa Baraza la Madiwani lililozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu.

Mkuu wa MMkoa wa Ruvuma ammewaonya wale Madiwani wote watakao Shirikiana na watendaji katika kujumu Halimashauri ya Tunduru kwa Namuna yoyote ile hatua kali zita Chukuliwa Dhidi yao kazi ya MMadiwani ni kuelekeza wanancchi kulima mazao yata kayo waongezea kukua kwa uchumi wao kamma Korosho Mbaazi na Choroko
 Viongozi wa Vyama vya Siasa wilaya ya Songea wakifuatilia kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Songea. Kutoka kulia wa kwanza ni katibu wa CCM wilaya ya Songea mjini anayefuata ni Katibu mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Songea Mjini na kushoto ni Katibu wa CUF wilaya ya Songea Mjini.
 Viongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika kikao cha Baraza la madiwani la Manispaa ya Songea katika ukumbi wa manispaa hiyo.
 Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Songea wakiwa katika kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani cha kumchagua Mstahiki meya na Naibu wake katika halmashauri hiyo. Kutoka kushoto ni Mweshimiwa Mariam Simba anayefuata ni Issack Lutengano, Katikati Shaibu Chitete diwani wa kata ta mjini, anayefuata Happy wa viti maalumu na mwisho ni Judith Mbogoro Diwani wa Viti Maalumu.
 Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Songea mara baada ya kuzinduliwa na mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu wakiwa katika picha ya pamoja na Mstahiki meya, naibu meya, mbunge wa Jimbo la Songea, mbunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma, Mkuu wa wilaya ya Songea na Madiwani wa Kata 21 za Manispaa ya Songea
 Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wilaya ya Songea Bw. Twaibu Chilumba amewataka wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia ipasavyo shughuli za maendeleo na kuwatumikia wananchi bila kujali itikadi za vyama kwa kuwa uchaguzi ulishaisha kilichobaki ni kazi tu.
 Maafisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Mama Lulandala na Bw. Nyakungu wakihakiki vocha za Pembejeo za Kilimo katika msimu wa kilimo wa 2015/2016 walipokuwa wakiwapatia wakulima pembejeo za mbolea za kukuzia katika ofisi za Kilimo wilaya ya Songea.
Meya wa Manspaa ya Songea Alhaji Abdull Hasani Mshaweji akitafakari hatma ya halmashauri ya wilaya ya wilaya ya Namtumbo.

No comments:

Post a Comment