KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, December 1, 2015

WAKULIMA WA JIMBO LA MADABA WAPEWA MBEGU ZA TANGAWIZI TANI SITA ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI ISHIRINI NA MOJA

  Mbunge wa Jimbo la Madaba Songea Vijijini Joseph Kizito Mhagama akiendesha Pikipiki

Katika Ziara yake pia Mh. Joseph Mwagama ameweza kugawa Pikipiki 3 pamoja na Baiskeli kwaajili ya mlemavu na Baiskeli nyingine  kupeleka katika kituo cha Afya Madaba.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mwagama kufanya ziara jimboni kwake toka alipochaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Madaba ambalo ni jimbo jipya.

  Mbunge wa Jimbo la Madaba Songea Vijijini Joseph Kizito Mhagama akiendesha Pikipiki
 Mbunge wa Jimbo la Madaba Songea Vijijini Joseph Kizito Mhagama akiendesha Pikipiki

Mbunge wa Jimbo la Madaba Songea Vijijini Joseph Kizito Mhagama amesema njia rahisi ya kuwainua Wananchi ni kutafuta mazao ambayo wakiuza yanaweza kutatua matatizo yao kwa haraka.
Mbunge wa Jimbo la Madaba ameyasema hayo wakati akigawa Tani sita za mbegu ya Tangawizi zenye thamani ya Shilingi Milioni 21 kwa wakulima wa Jimbo la Madaba ili wajiandae kulima zao la Tangawizi ambalo tayari limeshapata soko Nchini Kenya.

Mbunge wa Jimbo la Madaba Songea Vijijini Joseph Kizito Mhagama amesema Mazao ambayo yanaonyesha kuwainua wananchi kiuchumi ni kazi ya Viongozi kuwahimiza Wananchi kulima mazao hayo, kama Mbaazi, Aliseti, Maharage na Tangawizi

Mratibu wa Shirika la RUCODIA Ladislaus Bigambo amesema shirika lilianza na wanachama wakulima 300 lakini mpaka sasa wamefikia wakulima 2745, mbegu zilizopandwa wakati huo zilikuwa kilo 10 lakini sasa kuna Tani 9000.

 Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Kizito Mhagama akianisha miradi ambayo ana taka kuitekeleza katika jimbo la madaba huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Madaba Robeti Mageni

Wananchi wa Jimbo la Madaba wakipokea misaada hiyo wameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kulenga katika kuinua uchumi wa mtu wa kati kwa kutoa mbegu za Tangawizi na vitendea kazi.
Wamesema kukiwepo na Rasilimali Ardhi na watu wakipewa nyenzo Tanzania haikuwa miongoni mwa Nchi zinazolalamika na umaskini kwani mito ipo, maziwa yapo pamoja na mvua za kutosha, wamesema hivi sasa Tangawizi ya Tanzania inatakiwa sana Nchini Kenya pia baada ya kuipima imeonyesha ina ubora haina sumu ya kuweza kuwadhuru Binadamu.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Madaba akipokea Mbegu za Tangawizi kwa Mh.Joseph Kizito Mhagama

Mbunge wa Jimbo la Madaba Songea Vijijini Joseph Kizito Mhagama amesema Mazao ambayo yanaonyesha kuwainua wananchi kiuchumi ni kazi ya Viongozi kuwahimiza Wananchi kulima mazao hayo, kama Mbaazi, Aliseti, Maharage na Tangawizi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Madaba Robeti Mageni akiwa ameshika Tangawizi huku akimshukuru Mbunge wa Jimbo la Madaba kwa kutoa Tani 6 Zenye Thamani ya Shilingi milioni Ishirini na Moja

No comments:

Post a Comment