KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, December 1, 2015

UNAPO ZALIWA KATIKA MAISHA HAKUNA KITU KIZURI KAMA NDOA HEBU TUONE MKOANI RUVUMA KIJANA ABASI SAID KATIKA NDOA YAKE

Furaha iliyoje kuwa na Mke unaye Mpenda hapo ina onyesha kuwa ndiyo kwanza jua la Mapenzi lina Chomoza
 Kufunga ndoa kuna tegemea na Maisha uliyo ya rithi Mwislamu mara zote huhimizwa kuoa kwa kufua suna za Mtume Mohama Radhi ya mwenyezi Mungu iwe juu yake .Hapo Sheikh Issa Zawamba akifungisha ndoa kati ya Abasi Said na Farha Mursal komba
 Kijana Abasi Said akifikiri jinsi Mwenyezi Mungu alivyo mujalia hadi kuweza kufunga ndoa na kutimiza Suna za Mtumo Mohamad SW
                                Bwana Harusi Abasi Said akimuvisha Pete Bi Farha Mursal komba
 Furaha ni kitu ambacho kina takiwa kwa kila mmoja hapo bwana Harusi na Bi Harusi wakiwa katika furaha kuona kila kiltu kinacho takiwa na Mwislamu wame kitekeleza
 Mara chache kuona mwana mke ame mwegemea Mumewe jambo hili ni jambo ambalo lina takiwa kulitekeleza mara kwa mara,Unaambiwa kila unapo gombana na Mkewako fikiri kwanza siku ya Harusi na Ukumbuke watu walikuambia nini, Mara zote Hasira hukaa kifuani kwa Mpumbavu hivyo usifanye haraka kukasirika Mke ni Tunu uliyo pewa na Mwenyezi Mungu
 Mwenyezi Mungu amewaita watoto kuwa ni Malaika hivyo kila wakati uone mtoto mdogo ni nuru ya nyumba mukigombana jaribuni kumwangalia mtoto ana watafakari vipi. Huyo ni Acrama Abasi Saidi
 Acrama Abasi Saidi akiwa mitaa ambayo baba yake Abasi Saidi anako fanyia kazi Hebu angalia suti aliyo ivaa ina leta Raha huo ndio utunzaji wa Mtoto siyo mfedha kuishia kwenye anasa jaribu na wewe kuwekeza Pombe au anasa haita kuwa Benk yako hapo Baadaye bali Mtoto ni Hazina ya Kesho
 Kijana Njelela akiwa Msherekeshaji wa Ndoa ya Abasi Saidi ,Hii ni kutokana na Abasi Kuishi Vizuri na wenzake Mshahara wa wema ni ushirikiano Mungu awajalie Muendelee kupendana
                                Njelela akimpongeza kijana wake kwa kuweza kufunga ndoa
 Nikudura kupata mapenzi kama hayo wapo watu hawaja weza hata kukumbatiwa kiasi hicho
                                               Abasi Said akiwa na mkewe Bi Farha Mursal komba
 Wazee Hawa ni Wazee wenye Busara jaribuni kufuata Busara zao mkifanya Hivyo Maisha yenu yata kuwa Mepesi
 Vijana wangu mimi Adamu Mzuza Nindi nawatakia Maisha mema ila nawaomba Mkumbuke Furaha Hufunikwa na Chuki na Chukim ina tokana na Shetani Tafadhali Mkiona swala hilo Mkimbilieni mwenyezxi Mungu na kusema namkimbia shetani anaye pingwa na Mawe. Jaribuni kuwa na Marafiki Wazuri,Watu wenye Busara jitengeni na Kusengenya Watu Mungu kasema Mwenye kumsengenya Mwenzake ni sawa na kula Nyama ya Nduguye
 Kweli Ndoa huleta Furaha hebu ona hao watu waweili uta fikili ndiyo leo wamezaliwa la hiyo nifuraha iliyo jificha muda mrefu Njelela na Omary Chika walindeni Vijana wenu
 Baadhi ya watu walio shirikim katika ndoa hiyo niki mwona ndugu Omary Chika akiongoza jopo hilo
 Sheikh Issa Zawamba akisoma dua ya ndoa ambayo shabaha yake ni kuwajulisha watu wanao zunguka mji au wilaya kuwa julisha kuwa hawa watu wawili ni kitu kimoja pasitokee mtu kuvunja ndoa yao na kuhakikisha Mkono wa Mungu uko juu yao

No comments:

Post a Comment