KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, November 28, 2015

WANA RUVUMA WA SHIRIKI KATIKA SIKU KUMI NA SITA ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA KUTOA MICHANGO MBALIMBALI

 Kamishina wa Police ambaye ni Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela  akimukabidhi Mwenyekiti wa Dawati la Police Wanawake Mkude mchango wake kwa ajili ya kuweza kuwa saidia Watoto wanao ishi katika Mazingira Magumu
 Kauli mbiu ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia 2015
 Wageni waalikwa wakipokea salamu za wasanii.
 Maandamano ya Kupinga ukali wa kijinsia unaoendelea katika Jamii siku ya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukali huo mkoani Ruvuma.
 Mwenyekiti wa Dawati ambaye ni mratibu wakuandaa mipango itakayo weza kufanikisha Maadhimisho ya Siku 16 za ukatili wa kinjinsia Renatus Matias mkude akimuliza fedha zilizo patikana

 Katika vikao mbalimbali watu huweza kuchangia hoja wakati amelala usingizi hapo kiongozi mmpja wa juu ambaye ashugulia na maendeleo ya jamii akitoa hoja huku akiwa akitafakari

 Watoto wanahitaji kuhurumiwa dhidi ya adhabu kali
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Siku kumi nasita za kupinga ukatili wa kijinsia Mkoa wa Ruvuma Mwanasheria wa Serikali Renatus Mkude akifafanua mwenendo wa makosa ya kijinsia.

Katika kusheherekea siku kumi na sita za kupinga Ukatili wa Kijinsia Mkoa wa Ruvuma watoto zaidi ya watano walitupwa na watoto watatu kufa baada ya kukosa huduma muhimu.
Mwenyekiti wa Dawati la Polisi Wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo amesema ukatili dhidi ya Mtoto unatakiwa ushirikiano kwa jamii mzima kutokomeza ukatili huo.
 wadau wa dawati la kupinga ukatili wa kijinsia mkoani Ruvuma.
Mwenyekiti wa Dawati la Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo alitoa vyanzo kwa walemavu wawili ambao mmoja ni mlemavu wa mikono na mmoja ni mtoto ambaye anahitaji msaada wa kufanyiwa oparesheni ya kutoa maji kichwani, amesema tangu Dawati linatoa msaada kidogo lakini anawaomba Wadau mbalimbali kuweza kuchangia walemavu hao

Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amewataka Wananchi wote kushirikiana na Serikali katika kufichua vitendo vya Ukatili kwa Jamii yote.

 Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Dawati la Kupinga Ukatili wa kijinsia Mwanasheria wa Serikali Renatus Matias Mkude, katikati ni Mama Mdaula Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa siku kumi nasita za kupinga ukatili na kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela.
 wageni waalikwa wakiongozwa na Mgeni Rasmi Mama Mdaula na wageni waalikwa katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa Manispaa ya Songea.
 Watoto wanatakiwa kupewa haki za msingi ikiwa ni pamoja na kulindwa dhidi ya ukatili wa ain yoyote ili waweze kukua ipasavyo
 wanafunzi waliohudhuria katika Uzinduzi wa Siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia.
 wadau mbalimbali wa kupinga ukatili wa kijinsia, Kulia ni Mama Misango mtetezi wa Masuala ya msaada wa kisheria Manispaa ya Songea

Siku kumi na sita za kupinga Ukatili wa kijinsia Mkoani Ruvuma zitaambatana na kutoa misaada katika Vituo vya watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi.

 Katika Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia Mgeni Rasmi mama Mdaula aliweza kuwahamasisha wanafunzi wapende Elimu na kutambua umuhimu wa Elimu. pichani Mama Mdaula akisalimiana na wanafunzi katika Viwanja vya Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini Songea

Mwanasheria mkuu wa Serikali Mkoa wa Ruvuma Renatus Matias mkude alionyesha jinsi Serikali ilivyo makini katika kumlinda mtoto kuanzia akiwa tumboni.


Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia Farida Mdaula ameitaka Serikali kuchukua hatua kali kwa wale wote watakaopatikana na kosa la ukatili wa kijinsia wachukuliwe hatua kali. mgeni Rasmi Farida Mdaula katika sherehe hizo aliweza kulichangia Dawati la Police Wanawake kiasi cha  shilingi Milioni Mbili,

Mwenyekiti wa Dawati la Police Wanawake mkoa wa Ruvuma Anna Tembo aliainisha baadhi ya matukio yaliyofanyika wilayani Mbinga Mtu Mmoja ambaye aliwaua wapwa zake wata  kwakuwa chinja mmoja mmoja na hatimaye yeye mwenyewe kujinyonga.

 Pichani ni Matei Mukuru mlemavu wa mikono akiwa na mwenyekiti wa Dawati la Polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma. Matei ni Mtaalamu wa Kunyoa lakini ana changamoto ya kukosa vifaa vya kuweza kumsaidia katika shughuli hiyo. Hivyo anaomba wasamaria wema wamsaidia kiasi cha Tsh laki tisa ili aweze kununua mashine ya kunyolea na jenerata.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela akiwa na viongozi wa Dawati la Poli wanawake katika Ofisi za Dawati la Polisi Mkoa wa Ruvuma.
 Wajumbe wa Dawati la Polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma

Katika Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia Dawati litaweza kutoa Elimu katika Shule za msingi na Sekondari pamoja na kutoa Msaada kwa vituo vya kulelea Watoto yatima wadogo mjini Songea na Songea Vijijini pamoja na kutoa Msaada kwa Mzee Mlemavu ambaye ameshajichongea Jeneza atakalolitumia mara baada ya mungu kumchukua.

Wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia mkoa wa Ruvuma wakifuatilia matukio ya uzinduzi wa siku kuminasita za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa Mahend

No comments:

Post a Comment