KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, May 31, 2016

WADAU MBALIMBALI KUTOKA HALMASHAURI ZA MKOANI RUVUMA WAHAMASIKA KUUNGANA NA SHIRIKA LA PADI KATIKA KUWASAIDIA WAZEE.

 Shirika la PADI Tanzania limepanga kuwajengea Nyumba wazee wawili amb ao wanaishi katika mazingira hatarishi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo na wakuu wa Idara za halmashauri za Mkoa wa Ruvumas
 Wazee wa Mkoa wa Ruvuma wameishukuru Serikali kwa kuwajali kwa kutenga madirisha ya wazee na kuwatambua wazee kupitia Wizara ya Afya wamesema wanachosubiri ni sera ya wazee kutungiwa sheria itakayowalinda na ukatili dhidi yao.
 Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini wameahidi kutenga Bajeti kiasi cha sh. milioni 50.5 kwa ajili ya kuwezesha mikopo kwa wazee kupitia vikundi.
 Wadau wa masuala ya wazee kutoka Halmashauri za wilaya ya Songea Vijijini, Songea Manispaa na Halmashauri ya Madaba wameamua kutosubiri Bajeti za serikali kuu katika kuwasaidia wazee bali wameanza kuwashughulikia kupitia vyanzo vya ndani na fedha zao za mifukoni kwa kuchangia mahitaji ya wazee wasiojiweza.
 Wazee wa barabaza Huru la Wazee wa Manispaa ya Songea wameomba Jamii kutambua umuhimu wa wazee katika jamii zao wamesema wapo watu ambao bado wanawabeza wazee na kuwasingizia kujihusisha na imani za kishirikina.
 Watumishi wa shirika la PADI wakifuatilia hoja za wakuu wa Idara katika kupanga maazimio ya namna watakavyoweza kuwasaidia wazee kwa kushirikiana na Shirika la PADI.
 Watumishi wa Manispaa ya Songea katika kuhudumia wazee wamewezesha wazee 600 kuwaunganisha na Hospitali za Misheni za Mtakatifu Benedict matogoro na ya Mtakatifu Camilius Manispaa ya Songea kwa kuwalipia gharama za matibabu ambapo kila Zahanati hupeleka milioni tatu tatu kwa mwaka kwa ajili ya matibabu ya wazee. Pia katika bajeti ya 2016/2017 wametenga sh. milioni 50 kwa ajili ya kuwahudumia wazee kiuchumi na matibabu.
 Afisa Biashara wa Manispaa ya Songea akielezea namna atakavyotumia mapato yatokanayo na Biashara katika kuhakikisha wananufaisha na wazee kupitia vikundi vya ujasiliamali.
 Wakuu wa idara wa Manispaa ya Songea wakipanga mikakati ya kuwaingiza wazee katika Bajeti kutokana na Bajeti wanayoipata kwa kila idara. Wakuu hao wamejadili hayo wakiwa katika viwanja vya shirika la PADI Unangwa Manispaa ya Songea.
 Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri 3 za wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma walipokutana na wazee na Viongozi wa Shirika la Kuhudumia wazee la Padi na kuweka maazimio ya kuwasaidia wazee ikiwemo kutunga sheria ndogo ndogo katika kila Halmashauri za kuwalinda wazee.
Halmashauri ya Madaba imetenga Kiasi cha Shilingi Milioni 50,231,500 katika Bajeti ya 2016/2017 kwa ajili ya huduma za wazee  ikiwemo na kuwatengenezea vitambulisho vya matibabu.

No comments:

Post a Comment