KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, May 15, 2016

WAFANYA BIASHARA WACHANGIA MBAO 350 ZIKIWA NA THAMANI YA SHILINGI MILIONI NNE


WAFANYABIASHARA 4 WA BIASHARA YA MBAO MKOANI RUVUMA WAUNGA MKONO SERIKALI KWA KUICHANGIA MBAO 350 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 4 KWA AJILI YA UTENGENEZAJI WA MADAWATI


Mkuu wa wilaya ya Songea Benson Mpesya amewashukuru wafanya biashara hao  Asia Chakwela,Mussa Mwingira Ticson Luvanda na Rajabu Mbaja na kusema suala la utengenezaji wa Madawati ni la kila mmoja na siyo Serikali peke yake, Hivyo amewaomba wadau wengine waige mfano huo.




Afisa wa Wakala wa Misitu  Mkoa wa Ruvuma Manyisye Mpokigwa amesema kazi kubwa kwake  ni kuwahamasisha wafanya Biashara za Mbao kuungana na Serikali ili kupunguza tatizo la uhaba wa  Madawati.

Mwenyekiti wa Wafanya Biashara hao wanne Asia Chakwera amesema baada ya kutmbela Shul za Msingi mbili alipata uchungu kuona wanafunzi wakikaa chini ndipo alipowashauri wafanyabiashara wenzak kusaidia kutatua tatizo hilo

Wafanya Biashara wa Mbao Mkoa wa Ruvuma wameWameunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ya kuwataka wanafunzi wote ifikapo June 2016 wanafunzi wote wawe wanakaa kwenye Madawati.


Wafanya Biashara za Mbao wanne Mkoani Ruvuma wametoa Mbao zipatazo 350 zikiwa na Thamani ya Shilingi Milioni 4.4 kwa ajili ya utengenezaji wa madawati wilaya ya Songea.



Juhudi za Utengenezaji wa Madawati wilaya ya Songea hivi sasa unaenda kwa kasi karibu shule nyingi watoto wanakaa kwenye Madawati.

No comments:

Post a Comment