KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, May 18, 2016

WANANCHI WA KITONGOJI CHA NGUNGUTI KIJIJI CHA MUHUKURU SONGEA VIJIJINI WAMEIOMBA SERIKALI KUWASAIDIA KUMALIZIA UJENZI WA SHULE WALIYOIJENGA KWA KUJITOLEA NA KUWAPATIA WALIMU WA KUWAFUNDISHA WATOTO WAO.


Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya ambaye aliona taarifa kwenye Vyombo vya Habari kuhusu kutelekezwa kwa Shule ya Ngunguti iliyo katika Tarafa ya Muhukuru Songea Vijijini , amekanusha kuwepo kwa Shule hiyo bali kilichopo Wananchi wanahitaji watoto wao wapate Elimu, Serikali itafanya kila linalowezekana ili Shule iweze kusajiliwa


Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ngunguti amesema tayari wameweza kuandikisha watoto 30 na kumtafuta Mwalimu ambaye hana taaluma ya uwalimu ili aweze kuwafundisha watoto hao baada ya watoto kukosa Elimu kwa kipindi cha miaka saba kwa sababu ya shule hiyo kuto kusajiliwa.

 Moja ya changa moto inayo ikabili shule hii ya ngunguti  iliyo kilometa 176 ina  ukosefu wa madawati pamoja na ubao wa kuandikia watoto kama unavyo waona wana kaa chini hawana sare, Mkuu wa wilaya ya songea  Beson Mpesya ameahidi kuipa usajili pamoja na kuwa tafutia mwalimu wa muda wakati taratibu za usajili zikifanyika

Afisa Elimu Msingi wilaya ya Songea Vijijini Mtani Kameka amesema  wilaya ya songea vijijini haina shule inayo itwa ngunguti ila wanachi wamewakusanya watoto pamoja ili waweze kupata elimu hivyo gazeti { la uhuru }ililo andika habari hizo siyo kweli

 Wananchi wa kitongoji cha Ngunguti  songea vijijini kilometa 176 wakitoa mawazo yao kwa vyombo vya habari kuhusu maendeleo ya kitongoji hicho changamoto wanazo kabiliana nazo kuhusu Elimu na Afya ,Shule haina choo .uwanja wa michezo.hata walimu wenye taluma Serekari imeahidi kutatua matatizo hayo

Wananchi wa Kijiji cha ngunguti Kitongoji cha Ngunguti kijiji cha Muhukuru barabarani Songea vijijini wameiomba Serikali kuwasaidia Usajili wa Shule  pamoja na kuchangia vifaa  vya ujenzi ili waweze kumalizia Shule waliyoanza kuijenga.


Kijiji cha Muhukuru Barabarani kina Vitongoji 4 vyenye kaya 375 ambapo Kijiji hicho ni cha wakulima wakulima waliohamia kutoka wilaya ya Mbinga kwa kufuata rutuba kwa ajili ya Kilimo.

hII NI SHULE YA NGUNGUTI SONGEA VIJIJINI AMBAYO INA TEGEMEA NGUVU YA WAZAZI MPAKA SASA HAIJA SAJILIWA INA DAIWA KUWA NA WANAFUNZI 80 LAKINI WALIO JISAJILI WAPO 30

No comments:

Post a Comment