KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, May 29, 2014

SWALA LA UCHAGUZI KATIKA NCHI ZA AFRICA LA TAKA MOYO ,MACHO YETU MALAWI

Matokeo ya uchaguzi yatangazwa Malawi

Baadhi ya wagombea wa uchaguzi mkuu wa Malawi
Hatimaye Tume ya uchaguzi nchini Malawi imeanza kutoa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo jumanne iliyopita.
Matokeo hayo ambayo ni asilimia 30 tu ya kura ambazo zimehesabiwa hadi sasa yanaonyesha kuwa mgombea wa chama kikuu cha upinzani Democratic Progressive Party-DPP Profesa Peter Mutharika anaongoza kwa kura 683,621 akifuatiwa na Dr Joyce Banda wa Peoples Party kwa kura 372,101
Mgombea Urais wa chama kikongwe cha kisiasa nchini humo, Malawi Congress Party MCP Mchungaji Dr Lazarus Chakwera anashika nafasi ya tatu kwa kujipatia kura 289,145 huku Atupele Muluzi wa United Democratic Front- UDF akikusanya kura za wamalawi 269,250
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ambaye anafuatilia uchaguzi huo nchini humo, amesema mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mackson Mbendera aliwaambia waandishi wa habari mjini Blantyre usiku wa kuamkia leo kuwa tume yake kwa pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa wamethibitisha matokeo hayo.
Udanganyifu
Katika mkutano huo Jaji Mbendera amesema tume yake imegundua kuwa kulikuwa na udanganyifu katika baadhi ya maeneo ambapo wamekuta idadi ya kura zilizopigwa ni zaidi ya watu walioandikishwa kupiga kura, na kwamba wamezuia matokeo hayo hadi watakapo pata ufumbuzi na ukweli wa hali ilivyokuwa.
Wakati huo huo Mahakama nchini humo imezuia uamuzi wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la utangazaji la Malawi MBC kumlazimisha Mkurugenzi Mkuu Dr Benson Tembo kwenda likizo ya lazima na haraka.
Uamuzi huo umefuatia baadhi ya wanasheria kutoka kamisheni ya wanasheria wa Lilongwe kuweka zuwio mahakamani kupinga uamuzi wa bodi ya shirika hilo.
Itakumbukwa kuwa ijumaa asubuhi Dr Tembo alipewa barua ya kumtaka aende likizo ya lazima kutokana na madai kuwa ameshindwa kufuata maelekezo ya mwajiri wake ambaye ni serikali.
Miongoni mwa madai hayo ni pamoja na vyombo vya shirika hilo ikiwemo television na radio za taifa kuendelea kutoa matokeo ya uchaguzi ambayo hayajathibitishwa na Tume ya uchaguzi.
Pia MBC ilishindwa kurusha moja kwa moja matangazo ya mkutano wa Rais Joyce Banda na waandishi wa habari mjini Lilongwe siku ya alhamis, ambapo Dr Banda alikuwa akitoa maelekezo kwa tume ya uchaguzi kuanza kuhesabu kura kwa kutumia mikono na kuzuia kutoa matokeo kutokana na udanganyifu uliojitokeza.


Uchaguzi wa Malawi ulikumbwa na visa vingi vya wizi wa kura pamoja na udukuzi wa mitambo iliyokuwa inatumiwa kujumlisha kura. Haya ni madai ya Rais Joyce Banda.
Rais Joyce Banda ametaka kura hizo kuhesabiwa upya bila ya kutumia mitambo ya elektroniki ya kuhesabu kura.
Bi Banda alikumbwa na ushindani mkali katika uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumanne kutoka kwa wagombea watatu akiwemo, waziri wa zamani wa mambo ya nje Peter Mutharika.
Kwanini Waziri ajiue baada ya kijingiza katika uchaguzi ?
Mapema Alhamisi naibu waziri wa serikali za mitaa wa Malawi alijipiga risasi na kujiua nyumbani kwake mjini Lilongwe.
Godfrey Kamanya alikuwa anagombea kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Nzonzi Kusini.
Alijiua alfajiri ya leo katika mojawapo ya vyumba vya nyumba yake iliyopo Area Ten mjini Lilongwe.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali kuu ya Kamuzu mjini humo, na jeshi la polisi litatoa taarifa rasmi ya kifo hicho baada kukamilisha uchunguzi.
Haijajulikana sababu za Kamanya kujiua japokuwa ameacha barua ya maelezo ambayo polisi wataitoa baadae.
Matokeo ya kura bado hayajatangazwa rasmi katika kile kinachosemekana kuwa uchaguzi wenye ushindani mkali sana.
Afisa mkuu wa uchaguzi, amesema kuwa mfumo wa elektroniki umeharibika na maafisa wanatumia matokeo kwa njia ya barua pepe.

No comments:

Post a Comment