KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, April 17, 2016

KITENGO CHA HIFADHI YA CHAKULA (NFRA) SONGEA KIMELIINGIZIA TAIFA KIASI CHA TSH. 39,140,000,000 BAADA YA KUUZA MAHINDI TANI 103,000 KATIKA KIPINDI CHA 2015 2016.



Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea imefanikiwa kuuza Tani 103,000 za Mahindi katika Mikoa ya Tanzania iliyokuwa na Uhaba wa Chakula na kuweza kuliingizia Taifa kiasi cha Shilingi 39,100,000,000 kwa ajili ya uuzaji wa Mahindi. (Picha Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya akiwa na Meneja wa kitengo cha hifadhi ya Chakula Songea Bw. Amos Mtafya.

Hayo yamebainika wakati Naibu Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya alipokuwa akisomewa taarifa ya chakula kilichotolewa Mkoani Ruvuma kusaidia mikoa mingine yenye uhaba wa chakula Tanzania.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella  Manyanya alipokuwa katika hifadhi ya chakula Songea kununua Tani 5 za Mahindi kwa ajili ya wananchi wake waliopata Maafa ya Mafuriko katika Jimbo la Nyasa. 

Meneja wa Kitengo cha hifadhi ya Chakula (NFRA) Songea Amos Mtafya akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Elimu amesema katika kipindi cha 2015 – 2016 Hifadhi ya Chakula Songea imeweza kusafirisha Tani 88,000 kwa mikoa ya Tanzania bara yenye Upungufu wa chakula na Tani 10,000 kwa Shirika la  chakula Duniani (Word Food  Program– WFP) na Tani 8,000 kuhamishiwa katika Hifadhi ya Dodoma na Tani 5 kununuliwa kwa ajili ya watu waliopatwa na maafa jimbo la Nyasa na kitengo kimebakiwa na tani 11,000

Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya amesema miundombinu ya barabara na usafiri wa majini Serikali imeweza kusaini Mkataba wa kutengeneza Barabara ya Kitahi  -  Lituhi na Mbinga hadi Mbamba bay kwa kiwango cha lami.(Picha Gari ya Naibu Waziri ikiwa imenasa katika Tope akiwa ziarani Jimbo la Nyasa)

Nao wananchi wanaoishi vijijini wametakiwa kufuatilia kwa ukaribu Miradi inayofadhiliwa na Serikali, Miradi inayofanyika vijijini inatakiwa kuwa imara kusiwe na visingizio vya kujenga miradi chini ya kiwango kwa kudai ni miradi ya vijijini.


Mhandisi Stella Manyanya ameyasema hayo baada ya kuona Mradi wa ukarabati wa Kituo cha Afya cha kata ya Linga Wilayani Nyasa uliogharimu shilingi Milioni 27 simenti ya sakafu ikionyesha imepasuka kabla ya kumaliza mwaka mmoja.

Mhandisi Stella Manyanya amesema hakuna kisingizio cha kukarabati ovyoovyo miradi ya Vijijini na kusingizia miradi ya vijijini inatakiwa kulipua Wananchi wawe macho katika kusimamia miradi hiyo.(Pichani Mhandisi Stella Manyanya akikagua ukarabati wa Kituo cha Afya Litumba Kuhamba Kata ya Linga.)

Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya amesema katika Jimbo la Nyasa kutakuwa na mashindano ya ufaulu kubaini shule gani imefaulisha vizuri, mwalimu atakayeshindwa kufaulisha vizuri wanafunzi itambidi apishe nafasi hiyo ichukuliwe na wenzake watakaoweza kufundisha vizuri.Mh mhandisi Stela Manyanya ametoa agizo kiloa shule iwe na shamba darasa kwa ajili ya somo la kilimo

Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya akizungumza kuhusu Sekta ya Elimu amesema katika Tanzania kuna vyuo vikuu zaidi ya 50 na chuo kingine cha Madaktari bingwa wa Moyo na Mishipa ya Damu kinajengwa Mlogazila Dar Es Salaam ambacho kitachukua wanafunzi 15,000 wa fani ya Udaktar

Mhandisi Stella Manyanya amesema Serikali katika kuinua uchumi wa Watu wanaoishi Mwambao wa Ziwa Nyasa tayari mkataba wa kutengeneza Barabara ya Mbinga MbaMba Bay umeshatiwa sahihi kwa ujenzi wa kiwango cha lami.

Naibu Waziri wa Elimu amewahimiza Wazazi kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa kuboresha Elimu katika mambo yanayowahusu wazazi , kama kutoa chakula kwa watoto, Madawati pamoja na kuboresha eneo la kusomea.

Wananchi wa Maeneo yaliyopatwa na Maafa ya Mafuriko wamemshukuru Mweshimiwa Mbunge kwa kuweza kukimbia Jimboni na kutoa pole kutokana na Maafa yaliyowapata.

Akiongea na Wananchi wa Jimbo la Nyasa Mh. Naibu Waziri wa Elimu amesema ili uweze kuingia katika Vyuo hivyo unahitajika kufaulu vizuri kwa kupata Daraja la kwanza (Division One).

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu amesema pamoja na kurahisisha mawasiliano ya usafiri katika Ziwa Nyasa, pia ujenzi wa Bandari ya Ndumbi unaendelea,  na meli tatu zinaundwa, mbili zikiwa za mizigo na moja ya Abiria ambazo zitasaidia kusafirisha mizigo na Abiria kutoka Mbeya hadi Mbamba Bay.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Manyanya amesema wako watu wachache ambao wanawakatisha tamaa wenzao kuhusu Elimu, lakini watu hao ni wa kuwapuuza jambo muhimu kwa wazazi ni kutoa ushirikiano kwa Walimu kwa kuboresha Mazingira kwa kujenga Nyumba nzuri za walimu. 
Mheshimiwa Stella Manyanya alikuwa katika Ziara ya siku mbili katika Jimbo la Nyasa kwa ajili ya kutoa pole kwa wananchi waliopatwa na Maafa ya kukumbwa na Mafuriko.  

No comments:

Post a Comment