KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, April 25, 2016

WATU 144 WAKOSA MAHALI PAKUISHI BAADA YA NYUMBA ZAO KUANGUKA NA MVUA KUNYESHA MFULULIZO KWA SIKU TATU MKIOANI RUVUMA


Kaya 144 zimekosa mahali pakuishi katika Kijiji  cha Ngadinda Kata ya Gumbilo wilaya ya Songea vijijini baada ya nyumba 51 kubomoka na nyumba 91 kutetereka baada ya mvua kali kunyesha mfululizo  muda wa siku tatu mfululizo
Mkuu wa wilaya ya songea Bensoni Mpesya amesema licha ya nyumba kubomoka mvua pia imeathiri mashamba yapatayo  hekari 102 za nafaka mbalimbali zikiwemo mahindi mpunga na maharage
 Kufikia maeneo yenye maafa kunataka moyo hapo Gari la Mkuu wa wilaya ya Songea Bensoni Mpesya likiwa lime kwama na kusababisha mkuu huyo kutembea kwa mguu kukagua maeneneo yaliyo athirika katika kata ya Gumbiro

Mkuu wa wilaya ya Songea Bensoni Mpesya amesema maafa yaliyo tokea yametokea baada ya mto Hanga kufurika na kusababisha hasara kubwa lakini kamati ya maafa ya wilaya imejipanga kusaidia familia hizo katika ujenzi, chakula kipo cha kutosha
Mkuu wa wilaya ya songea Benson Mpesya amewaomba wananchi wa Songea ili kuepukana na majanga ya kubomokewa na nyumba wajaribu kufuata ushauri wa wahandisi wakati wa ujenzi, nyumba nyingi hubomoka kwa kukosa misingi imara

No comments:

Post a Comment