KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, April 5, 2016

TATHMINI YA MSAADA WA KISHERIA LUDEWA MKOANI NJOMBE


Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe Anatory Choya amewataka watu wanaotoa huduma ya Msaada wa kisheria kutumia taaluma yao kwa kutoonyesha mgogoro katika Jamii bali wajikite katika kutatua Migogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mkoani njombe ametoa Agizo hilo baada ya kuona kazi zilizofanywa na wasaidizi wa Kisheria kupitia Shirika Mashirika ya PADI na SOPCE kwa kutoa Elimu kwa Wananchi 59,876 na kutoa Mafunzo kwa Watoa huduma ya msaada wa kisheria 75 waliopo wilaya za Ludewa, Makete na Uwanging`ombe Mkoani Njombe.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Edward Haule amewaomba watoa Elimu ya kisheria kwa jamii kuwa na mawasiliano ya karibu na Ofisi ya Mwenyekiti wa halmashauri ya Ludewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa ili wanapotaka msaada waweze kupewa badala ya kulalamika mitaani.



Katika Tathmini ya katikati ya mradi katika kipindi cha miezi 15 iliyolenga kujua Mafanikio yaliyopatikana katika muhula wa kwanza, changamoto kubwa iliyojitokeza ni vitendea kazi katika Ofisi za wasaidizi wa kisheria kama Meza, Viti na vyombo vya usafiri ingawa Mradi umetoa viti vinne na meza moja kila ofisi ya wilaya pamoja na matumizi ya Stationaries Shilingi 20,000 kwa kila mwezi katika kipindi cha utekelezaji wa mradi.  

Mkurugenzi wa Shirika la PADI Iskaka Msigwa amesema katika Wilaya za Ludewa na Wanging`ombe  wasaidizi wa kisheria wameweza kusuluhisha ndoa zipatazo 200 na kutatua Kesi za Migogoro ya Ardhi zaidi ya kesi 80 bila gharama yoyote na kuwapa uelewa wananchi katika masuala yaMikgogoro ya Ardhi, Mirathi Masuala ya Unyanyasaji wa kijinsia pamoja na Elimu ya kujua Sheria kwa asilimia 80% katika wilaya zote.
Mkurugenzi wa PADI Iskaka Msigwa amesema kazi zote zinazofanywa na watu wa msaada wa kisheria ni kazi za kujitolea cha msingi wadau mbalimbali washirikiane kuweza kuwasaidia kwa nyanja mbalimbali.

Akiongelea Mafanikio ya Utoaji wa Msaada wa Kisheria Mkurugenzi wa Shirika la PADI amesema, Wanawake ambao walikuwa wakinyanyaswa kijinsia sasa wamepata Elimu ya kujitambua ikiwemo na mambo ya Ndoa na masuala ya migogoro ya mashamba.

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa amesema Wilaya ya Ludewa ni wilaya ambayo kijiografia imekaa kwa kuzungukwa na Milima, hivyo kwa jinsi mazingira hayo siyo rahisi Serikali kuwafikia wananchi wote lakini kwa kushirikiaana na Shirika la PADI na SOPCE kwa kuwatumia watu wa msaada wa kisheria wameweza kupunguza masuala madogo madogo ambayo yalitakiwa kutatuliwa na mabaraza ya Kata, Mahakama za Mwanzo na Ofisi ya Mkuu wa wilaya.

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kutoa ushirikiano kwa watu wanaotoa huduma ya msaada wa Kisheria katika Wilaya ya Ludewa kwa kuwapa Ofisi, kusaidia usafiri wanapokwenda vijijini kikazi pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na wasaidizi wa kisheria na wananchi kwa ujumla.
Wadau wa Masuala ya kisheria wamepongeza uwepo wa wasaidizi wa kisheria katika ngazi za chini kutokana na kukithiri kwa kesi za masuala ya ndoa, mirathi unyanyasaji wa kijinsia na masuala ya Ardhi ambazo wananchi walikosa fursa za kuyafikia mabaraza ya kata kutokana na kutojua sheria ama kwa kukosa fedha za kufungulia jalada mahakamani au kwenye mabaraza.

Katika Mila za wakinga na wabena wilaya ya Makete Mwanamke akijifungua hakuruhusiwa kulala juu ya kitanda pia hatakiwi kushiriki na Jamii chakula anachokula Mama aliyejifungua kikibaki ni lazima kimwagwe, kikiliwa kitaweza kuleta nuksi.
Jambo jingine Mama aliyejifungua haruhusiwi kulala Kitandani bali anatakiwa kulala juu ya nyasi ndogo ndogo na zitandikwe chini. Lakini hayo yote baada ya kupata Elimu ya msaada wa kisheria yametoweka ambapo Wilaya ya Ludewa wananchi 23496 wamefikiwa na elimu hiyo.
Wasaidizi wa msaada wa kisheria wameomba watendaji kuwapa ushirikiano pindi wanapokuwa vijijini wakitoa Elimu ya kisheria au kusuluhisha migogoro katika jamii.

Changamoto zingine zinazowakabili wasaidizi wa kisheria ni kukosa ushirikiano wa watendaji, kesi zote za migogoro ya Ardhi, Ndoa na misaada mingine hutatuliwa bure na watu wa msaada wa kisheria tofauti na Mabaraza ya Kata na watendaji ambao huomba chochote kwa wanaowatolea huduma.

Mratibu wa Mradi wa msaada wa Kisheria Wilaya za ludewa, Uwanging`ombe na Makete Mkoani Njombe Recho Steven amesema changamoto wanazokutana nazo wasaidizi wa kisheria ni pamoja na umbali wa maeneo ya kutoa msaada, mara zote hulazimika kutembea umbali wa kilomita hadi 30 kwa mguu.

Changamoto zingine ni kukosa ushirikiano wa watendaji, kesi zote za migogoro ya Ardhi, Ndoa na misaada mingine hutatuliwa bure na watu wa msaada wa kisheria tofauti na Mabaraza ya Kata na watendaji ambao huomba chochote kwa wanaowatolea huduma.
Jambo ambalo linaloongeza chuki na watendaji kuona sasa hawapati kesi za migogoro ya Ndoa, Mashamba na Mirathi baada ya wasaidizi wa kisheria kutoa Elimu ya kisheria na Jamii kujua huduma za kisheria ni bure.
Kutokana na Elimu inayoendelea kutolewa na wasaidizi wa kisheria katika wilaya za Makete, Ludewa na Uwanging`ombe migogoro ya Ardhi na kesi za ndoa zimepungua baada ya wananchi kufahamu haki zao na uelewa juu ya masuala ya kisheria.

Mratibu wa mradi wa kutoa Elimu ya Msaada wa Kisheria amesema watoa msaada kisheria walikuwa 75 lakini kutokana na changamoto za kujitolea watu wane walishindwa kuendelea na Mafunzo ya siku 25 yaliyotolewa na Shirika la PADI kwa kushirikiana na Shirika la SOPCE kwa ufadhili wa LPF.

No comments:

Post a Comment