KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, April 25, 2016

WAKULIMA HALMASHAURI YA MADABA WAMETAKIWA KUJIUNGA KATIKA VIKUNDI ILI WAWEZE KUNUFAIKA NA FURSA ZA MIKOPO YA PEMBEJEO NA KUWEZA KULIMA KILIMO CHENYE TIJA.


Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Madaba Prosper Luambano amewataka wakulima wa Halmashauri ya Madaba kujiunga kwenye vikundi ili waweze kukopa nyenzo za kulimia ikiwemo Matrekta.
Kaimu Mkurugenzi ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa kwa NMB kuwa waliweza kukopeshwa shilingi Milioni 113 na kuweza kulima kitaalamu Hekari zisizopungua Hekari 522 za Mahindi.

wakulima wa Halimashauli ya Madaba wakisikiliza watalamu wa kilimo njia za kuweza kuendelea kwa kutegemea kilimo
 Akina mama Madaba wamekiri kuwa kilimo kinaweza kuwa komboa baada ya kuvuna gunia 30 kwa ekari moja
 Pamoja na hayo wananchi wa madaba wameomba elimu ya kilimo ianze kufundishwa toka shule za awali ili mtoto aondoe dhana ya kusema masikini ndio wanao sitahili kulima

Nao Wakulima wamesema wameshindwa kupuliza dawa ya magugu kutokana na upungufu wa Vitendea kazi kama Mabomba ya kupulizia dawa, Wakulima wa madaba wamesema ili kilimo kiwe na tija wange weza kukopeswa mikopo ya muda mrefu kutegemea na zao unalo lilima


WAKULIMA HALMASHAURI YA MADABA WAMETAKIWA KUJIUNGA KATIKA VIKUNDI ILI WAWEZE KUNUFAIKA NA  FURSA ZA MIKOPO YA PEMBEJEO NA KUWEZA KULIMA KILIMO CHENYE TIJA.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba Prosper Luambano amesema ikiwa wakulima wataanza kulima kwa kutumia Trekta hali ya uchumi itaongezeka, amewaomba wakulima wa Halmashauri ya Madaba kulima pia zao la Tangawizi ambalo kwa Ardhi ya Madaba inakubali. Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba amewaomba wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwenye Kilimo waweze Madaba.

Wataalamu wa Kilimo wamewataka Wakulima wanapolima waangalie mbegu za kupanda ili wanapovuna wapate kujiwekea chakula na kupata kipato baada ya kuuza mazao yao watalamu hao wamewaomba wakulima kutumia dawa ya kuua magugu kwa kuwa ina punguza garama ya palizi


Mkoa wa ruvuma kwa msimu wa Mwaka 2015  - 2016 wanatarajia kuvuka lengo la mwaka jana  la kuvuna Tani  million 1.8 na kuweza kufikia Tani Milioni 2 kutokana wakulima kuelimika baada ya kupata elimu kutoka kwa watalamu  wa Mashirika ya RUDI na ACTN kupitia Makampuni ya SEEDCO, SYNGENTA na YARA. Kwa mwavuli wa Green Luvolation

No comments:

Post a Comment