KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, August 23, 2012

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA WAOMBA MSAADA WA ULINZI KATIKA MABWENI YA WASICHANA

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya wasichana Songea Welinald Riki Liwiki akieleza changamoto zinazo mkuta shuleni hapo ikiwa na bamoja na kuboka kwa wingo.Aidha amesema ingawa wanaume huingia shuleni hapo nyakati za usiku hakuna hata mwanafunzi mmoja aliye wahi kubakwa pia walimu wanasikia tu hawaja wahi kuwa ona wanaume hao

Adam Nindi Songea.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea wameiomba Serikali kuwaongezea ulinzi kutokana na kuingiliwa na Wanaume nyakati za usiku.

Mkuu wa Wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Songea Janemary Mwinyikombo amesema tabia ya kuvamia mara mara na wanaume imeongeza hofu ya wanafunzi na kusababisha wanafunzi kushindwa kujisomea nyakati za usiku.

Kiranja Mkuu wa Shule ya sekondari ya wasichana songea Janemary Mwinyikombo akiwa na Katibu Bernadetha Mathew Pamoja na Wanafunzi waliofanyiwa vitendo vya kinyama ikiwa ni pamoja na kuchaniwa nguo kwa wembe na Mwanaume ajulikanaye kwa jina la Ankol .ambaye mara kwa mara huingia kwa njia ya kimazingira wamesema hali hiyo inawakosesha raha shuleni hapo

Wamesema pamoja na wanafunzi kufunga milango na kupigilia misumari kwenye madirisha lakini cha kushangaza wanaume hao huingia na kuchana nguo za wasichana maeneo ya kifuani, wamesema hali hiyo hutokea kuanzia saa 7.00 usiku na pale wanapo ingia wanafunzi hukumbwa na hali ya kushindwa kusema.

Mwalimu Mkuu wa shule ya sekonndari ya wasichana Songea Welinald Riki Liwiki amekiri kuwepo kwa Vitendo hivyo na amesema ameongeza ulinzi, yeye mwenyewe pia anashiriki ulinzi, ameomba Jamii kushirikiana na shule katika kuwafichua watu wanaofanya vitendo hivyo kwa wanafunzi.

Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana songea amesema katika hali ya ulinzi wa usiku kwa kuwa naye hushiriki siku moja alinusurika kuuwawa na mlinzi baada ya mlinzi kufikili yeye ndiye mwanaume anaye waingilia wanafunzi kimazingira

Shule ya sekondary ya wasichana songea kwa miaka miwili mfululizo kumekuwa na vitendo vya wanaume kuwaingilia wanafunzi kimazingira ingawa hali hiyo bado ni tata wanafunzi a secondary ya wasicha wameomba jamii na wazee wa mila kukaa na kuweza kulitatua tatizo hilo vinginevyo itasababisha wanafunzi kuathirika zaidi kisaikolojia jambo litakalo sababisha elimu kuteremuka

No comments:

Post a Comment