KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, August 8, 2012

AMKATA MTOTO WAKE NA WEMBE KWA AJILI YA SHILINGI 1000

Na Noel Stephen Mpwapwa Dodoma

Mama mmoja aliye fahamika kwa jina la Grace Mahinyila amehukumiwakwenda jela miaka miatano baada ya kupatikana na hatia yakufanyiaukatili mwanae wa miaka 9.Mama huyo aliye mchanachana mwanae kwa viwembe sehemu mbali mbali zamwili wake kwa kile kinacho daiwa mtoto huyo alimwibia mama yake sh1000.

Akisomewa mashtaka mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama yawilaya Jemsi Kareyimaha na mwendesha mashtaka wa polisi ObeidLyafunyile mama huyo alikiri kosa na kuhukumiwa miaka mitano jela aufaini ya laki tatu na elfu hamsini ambayo aliikosa na kupelekwa jela.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni katika mtaa wa Hazina WilayaniMpwapwa kwa mama aliyefahamika kwa jina la Grace Mahinyila (40) kabilamhehe kazi mkulima, kwa kumchanachana mwanae sehemu mbalimbali nakiwembe kwa kile anachodai amechoshwa na Tabia ya mwanae ya uwizi.

Akiulizwa mbele ya polisi mama huyu alikili kutenda kosa hilo na kudaikuwa mwanae huyo anatabia ya uwizi,kitu alichosema kina mkasirishasana.Polisi Wilayani Mpwapwa kupitia Dawati la njinsia WP Asia 8513alisema kuwa Baada ya kumkamata bi Grace alikili na alifunguliwajalada na amehukumiwa miaka (5) jela kwa kosa la kumjeruhi mwanaekinyume na sheria ya mtoto ya mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment