KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, March 24, 2013

ASIKARI POLICE ALIYE UA MKOANI RUVUMA NAYE AUWAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KARI



AJIRA YA JESHI LA POLICE  IENDANE NA MAADILI YA UKOO WA MWAJIRIWA.

Adamu Mzuza Nindi - Songea

Kwa namna ya pekee napenda kutoa pole kwa Familia ya Askari wa Jeshi la Polisi P.C. Yohana aliye uwawa na Raia wenye hasira kari baada ya asikari huyo kumpiga risasi Mkisio Ngonyani 27 aliye pakizwa na dereva wa bodaboda na yeye kuuwawa na wananchi wenye hasira kali  .wote wawili walipatwa na mkasa huo katika Kijiji cha Kwinde Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma.

Kwa mujibu wa tarifa zilizo tolewa na kamanda wa police Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki zina sema Mkasa huo ulimpata asikari huyo baada ya kumsimamisha dereva wa bodaboda ambaye alipakiza watu wawili kinyume cha sheria, lakini dereva huyo hakuweza kusimama ndipo Asikari Police  Pc Yohana  number 7771 alipo inua bunduki na kufyatua risasi iliyo mpata Makisio Ngonyani kichwani na kufa papo hapo.

Wananchi wamekuwa wakichukua Sheria mkononi kutokana na Busara zinazofanywa na Askari wa Usalama Barabarani.

Ukiangalia tukio lililotokea Ngwinde ni tukio ambalo linatakiwa Askari kujishauri kabla ya kufanya Tukio la Mauaji.

Mtuhumiwa amebeba Abiria wawili na umemsimamisha haja simama, jambo la Busara ni kunukuu Namba halafu Mtuhumiwa atafutwe, lakini unapofyatua risasi, risasi hiyo inaweza kumpiga raia ambaye hana hatia. Jee wale walio kuwepo wanakuwa na Mawazo gani ?

Ningeshauri nikiwa Raia wa Tanzania kabla ya Askari hajapata Ajira Jopo la wanaomteua basi walau wajue Tabia ya Mtu huyo kabla ya kuajiriwa, kujua Tabia ya Ukoo inaweza kusaidia kupata Askari Bora.

Upande wa Wananchi Tunapoamua kuingia Barabarani kuendesha Vyombo vya Moto ni lazima tujue hatuko juu ya Sheria ni lazima tufuate Sheria, kwenda kinyume cha Sheria Tuone kuna tunalazimisha vyombo vya Dola kutumia Sheria  na Sheria zingine ni hizi zinazosababisha vifo kwa Raia.

Wananchi wenzangu ni lazima tuwe tunasahihisha yale Mabaya yanayotokana na Ubongo wetu kuutumia vibaya kuna methali isemayo you must think before doing the things. Mitihani haisahihishwi shuleni tu hata katika ubongo wa binadamu tuna takiwa kuwa na kawaida hiyo

Watu wanachoangalia ni kifo cha mtu na siyo kufikiri jinsi ya kuepuka Vifo hivyo.

Wananchi tujitahidi kufuata Sheria ili kuweza kulinda Roho zetu.  

No comments:

Post a Comment