KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, March 6, 2013

KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUVUMA YA BAINIWANAFUNZI WALIOFAULU KUSHINDWA KWENDA SHULE

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya  kutafuta Mbinu mwafaka ya kuhakikisha wanafunzi waliofaulu Mtihani wa Darasa la Saba kwenda Kidato cha kwanza wanaripoti Shule walizopangiwa.

Mkoa wa Ruvuma kati ya Wanafunzi 30,555 waliofanya Mtihani wa Darasa la Saba, Wanafunzi 16,578 waliweza kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza lakini walioweza kuripoti na kuanza Masomo ni Wanafunzi 9798 Wanafunzi 6665 hawajaweza kuripoti Shuleni mpaka sasa.
Katibu Msaidizi wa Maadili Kanda ya Kusini Muhuwa Kapangawazi amewataka Viongozi kutekeleza yale waliyo wahaidi Wananchi, hiyo ndiyo itakayo onyesha Maadili mema kwa Wananchi wanao watawala.
Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Ruvuma wameshauri Bajeti zinazotengwa kwa H/za Wilaya  zitangazwe baada ya kufika mikononi mwa Wakurugenzi, kutangaza kabla ya kuwafikia Wakurugenzi ni kuwachonganisha na Wananchi wakidhani Wakurugenzi wamekula Fedha hizo.
Mjumbe wa Ushauri Mkoa wa Ruvuma Jenista Mhagama amesikitika na Mipango inayo kwamisha kufikisha Maendeleo kwa Wananchi, akitoa mfano amesema Banki ya Maji ya Dunia ilitoa kiasi cha Shilingi Milioni 200 mwaka 2003 ili mradi huo utekelezwe kwa kupeleka Maji katika Vijiji vya Maweso lakini mpaka sasa mradi huo haujafanyika.

No comments:

Post a Comment