KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, March 8, 2013

UHURU KENYATA ASHINDA U RAIS KENYA

UHURU KENYATA AKIWA KATIKA KAMPENI
 Guys im shoo happy wallah and i would like to announce kwamba UHURU KENYATTA ndio Rais mpya wa Kenya.
Kenyatta ameshinda kwa kura 6,173,433 ambayo ni sawa na asilimia 50+1 na kumuacha mbaliii mpinzani wake Raila Odinga.. Matokeo rasmi yatatangazwa kesho saa 5 asubuhi..
From my heart naandika uku machozi ya furaha yananitoka, THIS MAN UHURU KENYATA IS young, wild and free president...i got something to learn from HIM!!
KILA LA KHEIR MR PRESIDENT!!
UHURU KENYATA AKIWAZA KAMPENI, HATIMAYE ASHINDA
MTOTO wa Rais wa kwanza wa Kenya, Marehemu Rais Jomo Kenyatta, ambaye alikuwa anagombea Urais kwa tiketi ya Chama cha TNA, Uhuru Kenyata ameshinda nafasi hiyo baada ya kumwangusha mpinzani wake Raila Odinga.

Hadi saa 8:35 usiku wa leo Uhuru alikuwa mbele kwa kura 6,173,433 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliyekuwa na kura 5, 340,546 ikiwa ni tofauti ya kura 832,887 na majimbo yaliyo kwisha kutangazwa ni 291/291.

Jumla ya kura zote zilizopigwa na kuhesabiwa kwa nafasi ya Urais ni kura 12,338, 667 kutoka katika majimbo yote ya Uchaguzi 291 huku kura zilizoharibika zikiwa 108975 na kura halali zikibaki 12,222,980.

Katika kinyang’anyiro hicho Wycliffe Musalia Mudavadi anashika nafasi ya tatu akiwa amejikusanyia kura 483,981 nafasi ya nne ikienda kwa Peter Kenneth mwenye kura 72,786.

Mgombea wa Alliance for Real Change,Mohamud Abduba Dida anashika nafasi ya tano akiwa na kura 52,848 akifuatiwa na Mwana mama Martha Karua wa National Rainbow Coalition mwenye kura 43,881 hadi sasa.

Nafasi ya saba katika wagombea hao Urais inakwenda kwa James ole Kiyiapi wa Chama cha Restore and Build Kenya ambaye ana kura 40,998 huku nafasi ya ya nane na mwisho ikishikwa na Paul Kibugi Muite wa chama cha Safina
.

No comments:

Post a Comment