KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, March 25, 2013

UJIO WA RAISI WA CHINA UNA FAIDA GANI KWA TANZANIA ?


Na  Adam  Nindi,  Songea

 UJIO WA RAIS WA CHINA NCHINI TANZANIA UNATUKUMBUSHA MENGI:

Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ujio wa Rais wa China unatukumbusha mambo mengi, mambo hayo ni pamoja na Ujasiri, Huruma,
 Kuthubutu pamoja na kujiamini kuwa kila kitu endapo utakipanga vizuri kinawezekana.

Wakati wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema Hakuna Mnyororo ambao unaweza kumkomboa Mtanganyika ni Ujamaa pekee.

Sera ya Ujamaa ilitokana na Rais wa China wa wakati huo Mao Satuni ambaye aliweka mikakati kwa Wananchi wa China kufanya kazi kwa pamoja jambo ambalo limewapa Ufanisi.

Tanganyika wakati huo kufuatia Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea iliweza kupiga hatua, Ujamaa ulianza JKT hadi kwa Wananchi ambao walikuwa na mashamba ya pamoja au kundi Fulani kujikusanya na kulima Shamba la mtu mmoja.

Kinachotakiwa kwa sasa, tunatakiwa kuangalia Jee hawa wenzetu wa China toka tuachane kipi kimewapa Ufaulu. Jee Watanzania tufanyeje tusiishie kupiga Ngoma na Ngonjera nyingi huku tukiwa hakuna tunachojifunza.

Kipindi cha Mwalimu Nyerere tuliiga Mvao wa watu wa China ya chonlai, pia Ujamaa halisi.

Hivyo kufika kwa Rais wa China kuwe ni ufunguo wa kuweza kupata Maendeleo.  

Rais wa China  Xi Jiping mara baada ya kuwasili nchini Tanzania  akiahidi kuto ingilia mambo ya ndani ya Nchi bali ita weza kuto mikopo yenye unafuu kwa Nchi za Afirica

No comments:

Post a Comment