KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, March 4, 2013

WAISHIO MPAKANI MWA ZIWA NYASA WAISHI KWA AMANI

Sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Malawi ni Rangi Nyekundu inayo onyesha pembeni mwa Ziwa Nyasa ,Alama kamili msitari huo unge pita katikati ya Ziwa Nyasa

Hakuna mgogoro wa mpaka Tanzania na Malawi-Serikali

Na Mwandishi Wetu,Dodoma

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rita Mlaki, aliliambia Bunge jana kuwa hakuna mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi unaosababishwa na Ziwa Nyasa.

Alisema wameshakaa vikao mara mbili na viongozi wa serikali ya Malawi kuzungumzia kuhusu mipaka na kuridhika kuwa hakuna tatizo hilo kati ya nchi hizo.

Waziri Mlaki alisema wanatarajia kukaa kikao cha tatu ili kupata tafsiri ya namna mipaka inavyogawanywa katika maeneo ya ziwa na bahari.

Alikuwa kijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mkwajuni (CCM), Mzee Ngwali Zuberi, aliyetaka kujua lini serikali za Tanzania na Malawi zitakaa kutatua tatizo la mipaka kati ya nchi hizo.

Swali hilo lilitokana na swali la msingi la Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kwa Waziri wa Maji, aliyetaka kujua serikali imeshindwaje kunadi jina la Ziwa Nyasa ili kuondoa utata wa Malawi inayodai kuwa ziwa hilo lote ndani ya nchi yao.

Naibu Waziri wa Maji, Shamsa Mwangunga akijibu swali la Mbunge Nyalandu alisema Tanzania ina uhusiano mzuri na Malawi kwa muda mrefu na kwamba ahaina mgogoro kuhusu ziwa hilo.

Hata hivyo, alikiri kuwa sheria za wakati wa wakoloni ndiyo chimbuko la Ziwa Nyasa na kwamba mkataba wa Anglo German ulibainisha kwamba ziwa hilo ni milki ya Malawi kinyume na taratibu za sasa za mipaka inayopita majini, inayotoa fursa sawa kwa nchi zinazotenganishwa kwa ziwa au bahari, kwamba mpaka upitie katikati ya ziwa au bahari husika.

Alisema Tanzania na Malawi zinaendelea kutumia ziwa hilo kwa shughuli za kila siku bila ya mgogoro wa aina yoyote na pia zinaendelea kubuni miradi ya pamoja ya kuendeleza Bonde la Ziwa Nyasa.

No comments:

Post a Comment