KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, December 4, 2013

TUFANYEJE ILI KUINUA KIWANGO CHA UCHUMI KATIKA ZIWA NYASA

 Umasikini unao tokea katika ziwa nyasa una tokana na zana duni za kuvulia wananchi wana mwamuko wa kuvua samaki dagaa pamoja na samaki wa mapambo wakila namuna, lakini jambo ambalo ni kikwazo ni kukosa utalamu, pia vifaa vya kuvulia samaki ziwa hili la nyasa kila siku zaidi ya Tani 2 hurudishwa Baharini wavuvi wakiogopa kuzama kutokana na uzito, Tushirikiane tutumie mbinu gani kuweza kukabiliana na hali hii ?
 Hapo baadhi ya wakaazi waishio mwambao wa ziwa nyasa wakiwa kandokando mwa ziwa Nyasa wakiburudika kwa vinywaji mbalimbali lakini hakuna Majumba ya fahali mbayo yanaweza kuwa vutia watalii ni juu ya kila mtu aliye zaliwa mwambao wa ziwa nyasa kuja kujenga nyumbani kwao badala ya kulowea katika miji ya wenzao .
Kama unavyo ona meli hiyo MV Songea inatokea Malawi ambako wenzetu wa Malawi wanalitumia vizuri Ziwa hili wamejenga vitega uchumi vingi lakini ona Meli yetu imetuwama kando kando mwa Ziwa Nyasa huku
 Ndugu yangu mimi naitwa Adamu Nindi Tukishirikiana na Judidhi Lugoye kujaribu kuanisha Maendeleo ya wenzetu na sisi tulioko pembezoni mwa Nchi hasa huku kusini kunako julikana kama kusini mwa Tanzania au Songea, Ninacho taka kuwa ambia nikuwa hata Roma haiku jengwa siku moja hata hapa Arusha nilipo simama hapo awali hapa kuwa hivi jee tufanyeje ili tufike hapa
 Swala nililelille hapa ni Dar es Salaam Mikwecheni katika Hoteli ya May Fair Hotel hivi ni vitega uchumi vilivyo jengwa na wazawa jee sisi huku Nyasa hatuwezi kujenga vitu kama hivi naomba watu wa Ruvuma tujaribu Kuthubutu tuta weza naweka picha hizo ili tuweke wivu wa kuthubutu


 AICC ni moja ya kumbi ambazo kuna fanyika Mikutano ya kimataifa kutokana na ukaribu wa Nchi za Afirika Mashariki lakini Mkoa wa Ruvuma nao una Nchi jirani kama Musumbiji ,Malawi,Zimbabwe hata Boswana Endapo atatokea Mwekezaji kujenga Songea kumbi kama za AICC Zita kuwa na ubora na kuongeza uchumi wa Kusini
 Kama kuna watu wana jua kuangalia Madhali una weza kuona jinsi Ziwa nyasa linavyo Vutia karibu mkoa wa Ruvuma uwekeze kuna vivutio vingi ,Milima ya Livingstone, Mawe ya Mbuji yanayo tumika kwa ibada ya kuomba mvua au majanga yakitokea, Pia kipo kisiwa ambacho kilitumika wakati wa vita vya kwanza na vita vya pili vya Dunia kisiwa hicho kilikuwa na uwezo wa kuhifahi watu 250 ni hicho kinacho onekana kwa mbali mkono wa kushoto
 Mwandishi mwandamizi ndugu Ayoub Rioba akitoa mada  jijini Arusha jinsi Vyombo vya habari vinavyo saidia kujenga nchi na kuiweka Nchi kuwa kiganjani,
 Hapo ni Dar es Salaa jee sisi watu wa mwambao Tuta fikia hali hiyo ? Najua weazawa kwa changamoto hizi watafanya kitu
Ukaaji huu wa chini siyo kuchoka bali ni kutafakali mikakati iliyo tumika kuendeleza miji hii jee viongozi tulio nao wanaona changamoto hizi, au kazi kubwa ni kukimbia kwao na kwenda kulala mijini, Ndugu yangu nikupe kisa mkasa Mtu mmoja huku kusini alikuwa Mtu mkubwa sana na mwenye hela katika wasiya wake aliandika kuwa akifa aka zikwe kwao ndugu yangu Jeneza lilipo fika lilikuwa lina shangaa Nyumba na Nyumba lilikuwa likishangaa Jeneza  Sanduku lilishindwa kuingia ndani kutokana na Mlango kuwa Mdogo usiombe kukuta na hali kama hiyo jaribu kujijenga hivi sasa
Nimekaa chini na Jamii ya Kimasai jijini Arusha lakini nilicho jifunza nikuwa hawa watu wana jali sana mila na desituri, Pia kivutio kikubwa kwao ni kuzungumuza lugha muda wote kutokana na hilo huitwa kila mgeni anapo fika na kuimba kwa lugha yao na kuongeza kipato, Jee sisi huku kusini watoto wangapi wana jua kingoni,au kimatengo na hata kindendeule kwa mtazamo huo tuna enda wapi, Aaa na Upenda Mkoa wa Ruvuma

No comments:

Post a Comment