KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, March 29, 2013

MAZOEZI HUONGEZA MDA WA KUISHI KWA WAZEE NA VIJANA

 
Moja ya mambo yanayo sababishi vifo vya kwa wazee ni kukosa kushiriki Mazoezi ya viungo  jambo linalo wa sababishia wazee kuwa jalala la magonjwa mbalimbali , katika nchi zinazo endelea zina mashine ya mazoezi ,Vijana wazee hushiriki katika mazoezi .Tanzani kuna sehemu chache zenye mashine hizo ,watu wanao bahatika kupanga hoteli kubwa hupata bahati ya kufanya mazoezi kama anavyo onekana ndugu Adamu Nindi akifanya zoezi Blue Pearl jijini Dar – es –salamu
 Hapo ndugu Adamu Nindi ambaye ali hudhulia Semina ya Gender Protoco Jijini Daer - es - salaam. kila jioni alikuwa akifanya mazoezi kama anavyo onekana katika picha
 Moja ya njia ya kujipima misuri ni mashine hiyo unayo iona Mbele yako  katika Hotel ya Blue Pearl
 Baada ya mtu kukimbia kilometa kaza ,kuna kuwa hakuna haja ya kukimbia mwendo mrefu una weza kukimbia kwa kutumia mashine kama anavyo onekana ndugu Adamu Nindi katika Hotel ya Blue Pearl
Mara baada ya kufanya mazoezi unatakiwa kuweka mwili wako katika hali mzuri hapo ndugu Adamu Nindi akijitayarisha kuogelea katika Swimming pool la Hotel ya Blue Pearl
Swimming Pool inayo onekana hutumika kwa wateja walio panga katika Hotel ya Blue Pearl  ili kuweka miili yao katika hali nzuri

Wednesday, March 27, 2013

MKUTANO MKUU WA SADC GENDER PROTOCOL



 Naibu waziri wa Maendeleo  ya Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu ameyasema hayo wakati akifungua semina ya siku moja kuhusu Mrejesho wa Genda Protocol  ambayo umehusihsha wandishi wa na wadau mbali mbali kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi
 Naibu waziri wa Maendeleo ya Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amewataka wanawake kujitokeza katika ugombea madarkaka mbalimbali ili wakifanikiwa waweze kutetea haki ya mwanamke na Watoto.
 Washiriki katika semina ya kutathiminimambo yaliyo fanyika kupitia Gender Protoco ambayo ina fanyika katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel jijini Dar -es-salaam
washiriki katika semina ya Gender Protoco wakiwa wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Naibu waziri wa Mendelo ya jinsia na watoto Ummy Mwalimu akiwa ukumbi wa blue Pearl 
 washiriki katika mkutano wa Sadc wakiwa jijini Dar- es -salaam wapili kutoka kushoto ni mwakilishi waakinamama kutoka mkoa wa Ruvuma mama Lwambano
 Mwenyekiti wa Gemsa Gladines Muuno akiwa na Naibu waziri wa Maendeleo Jinsia na watoto Mh.Ummy Mwalimu
 Mwalishi ambaye ni Mwandishi akibadilishana mawazo na Mjumbe kutoka Ruvuma mama Lwambano
 Picha ya Pamoja iliyo pigwa pamoja na Naibu waziri wa Maendeleo jinsia na Watoto akiwa na wajumbe wa SADC katika ukumbi wa Blue Pearl
 Naibu waziri wa Maendeleo Jinsia na Watoto akiwa katika Picha ya Pamoja na Afisa Uhusiano wa TGNP l
Viongozi wa andamizi wa Sadc wakishiriki semina ya kuhusu utathimini wa Gender Protoco mafanikio na Mapungufu yaliyo jitokeza kwa kipindi hiki kifupi

Wajumbe mbalimbali wakijiandikisha kushiriki semina ya Gender Protoco iliyo husisha wajumbe kutoka SADC
Wajumbe wakijiandikisha katika ukumbi wa Blue Pearl jijini DSM
Wandishi wa Habari wakiwa katika harakati za kutuma habari za kuhusu unyanyasaji wa kijinsia baada ya Hotuba ya Naibu waziri wa Maendeleo jinsia na watoto
wajumbe kutoka Tanzania kisiwani wakiwa ndani ya ukumbi wakingoja semina
Mwakilishi wa GEMSA Adam Mzuza Nindi kutoka Mkoa wa Ruvuma akiwa na mama Lwambano wakijadili jinsi ya kufikisha ujumbe wa Gender Protoco kwa watu walioko pembezoni hasa waqnanchi wa mkoa wa Ruvuma
Wajumbe kutoka Tanzania visiwani wakiwa na wajumbe kutoka Tanzani Bara wakibadilishana mawazo kuhusu ukatili wa kijinsia ulivyo Tanzania bara na Tanzania Visiwani
Juma Nyumayo na Mama Lwambanowa kifikiria changamoto zinazo patikana Mkoani Ruvuma


Monday, March 25, 2013

UJIO WA RAISI WA CHINA UNA FAIDA GANI KWA TANZANIA ?


Na  Adam  Nindi,  Songea

 UJIO WA RAIS WA CHINA NCHINI TANZANIA UNATUKUMBUSHA MENGI:

Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ujio wa Rais wa China unatukumbusha mambo mengi, mambo hayo ni pamoja na Ujasiri, Huruma,
 Kuthubutu pamoja na kujiamini kuwa kila kitu endapo utakipanga vizuri kinawezekana.

Wakati wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema Hakuna Mnyororo ambao unaweza kumkomboa Mtanganyika ni Ujamaa pekee.

Sera ya Ujamaa ilitokana na Rais wa China wa wakati huo Mao Satuni ambaye aliweka mikakati kwa Wananchi wa China kufanya kazi kwa pamoja jambo ambalo limewapa Ufanisi.

Tanganyika wakati huo kufuatia Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea iliweza kupiga hatua, Ujamaa ulianza JKT hadi kwa Wananchi ambao walikuwa na mashamba ya pamoja au kundi Fulani kujikusanya na kulima Shamba la mtu mmoja.

Kinachotakiwa kwa sasa, tunatakiwa kuangalia Jee hawa wenzetu wa China toka tuachane kipi kimewapa Ufaulu. Jee Watanzania tufanyeje tusiishie kupiga Ngoma na Ngonjera nyingi huku tukiwa hakuna tunachojifunza.

Kipindi cha Mwalimu Nyerere tuliiga Mvao wa watu wa China ya chonlai, pia Ujamaa halisi.

Hivyo kufika kwa Rais wa China kuwe ni ufunguo wa kuweza kupata Maendeleo.  

Rais wa China  Xi Jiping mara baada ya kuwasili nchini Tanzania  akiahidi kuto ingilia mambo ya ndani ya Nchi bali ita weza kuto mikopo yenye unafuu kwa Nchi za Afirica

Sunday, March 24, 2013

ASIKARI POLICE ALIYE UA MKOANI RUVUMA NAYE AUWAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KARI



AJIRA YA JESHI LA POLICE  IENDANE NA MAADILI YA UKOO WA MWAJIRIWA.

Adamu Mzuza Nindi - Songea

Kwa namna ya pekee napenda kutoa pole kwa Familia ya Askari wa Jeshi la Polisi P.C. Yohana aliye uwawa na Raia wenye hasira kari baada ya asikari huyo kumpiga risasi Mkisio Ngonyani 27 aliye pakizwa na dereva wa bodaboda na yeye kuuwawa na wananchi wenye hasira kali  .wote wawili walipatwa na mkasa huo katika Kijiji cha Kwinde Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma.

Kwa mujibu wa tarifa zilizo tolewa na kamanda wa police Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki zina sema Mkasa huo ulimpata asikari huyo baada ya kumsimamisha dereva wa bodaboda ambaye alipakiza watu wawili kinyume cha sheria, lakini dereva huyo hakuweza kusimama ndipo Asikari Police  Pc Yohana  number 7771 alipo inua bunduki na kufyatua risasi iliyo mpata Makisio Ngonyani kichwani na kufa papo hapo.

Wananchi wamekuwa wakichukua Sheria mkononi kutokana na Busara zinazofanywa na Askari wa Usalama Barabarani.

Ukiangalia tukio lililotokea Ngwinde ni tukio ambalo linatakiwa Askari kujishauri kabla ya kufanya Tukio la Mauaji.

Mtuhumiwa amebeba Abiria wawili na umemsimamisha haja simama, jambo la Busara ni kunukuu Namba halafu Mtuhumiwa atafutwe, lakini unapofyatua risasi, risasi hiyo inaweza kumpiga raia ambaye hana hatia. Jee wale walio kuwepo wanakuwa na Mawazo gani ?

Ningeshauri nikiwa Raia wa Tanzania kabla ya Askari hajapata Ajira Jopo la wanaomteua basi walau wajue Tabia ya Mtu huyo kabla ya kuajiriwa, kujua Tabia ya Ukoo inaweza kusaidia kupata Askari Bora.

Upande wa Wananchi Tunapoamua kuingia Barabarani kuendesha Vyombo vya Moto ni lazima tujue hatuko juu ya Sheria ni lazima tufuate Sheria, kwenda kinyume cha Sheria Tuone kuna tunalazimisha vyombo vya Dola kutumia Sheria  na Sheria zingine ni hizi zinazosababisha vifo kwa Raia.

Wananchi wenzangu ni lazima tuwe tunasahihisha yale Mabaya yanayotokana na Ubongo wetu kuutumia vibaya kuna methali isemayo you must think before doing the things. Mitihani haisahihishwi shuleni tu hata katika ubongo wa binadamu tuna takiwa kuwa na kawaida hiyo

Watu wanachoangalia ni kifo cha mtu na siyo kufikiri jinsi ya kuepuka Vifo hivyo.

Wananchi tujitahidi kufuata Sheria ili kuweza kulinda Roho zetu.  

Tuesday, March 19, 2013

UTUNDIKWAJI WA MIZINGA WA FANYIKA NAIKES RUVUMA

 Wananchi wanaoishi Vijijini Mkoani Ruvuma wametakiwa kujiongezea zao la biashara kwa kuanza kufuga nyuki badala ya kuwa na Mazoea kutegemea zao moja la Biashara.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu ameyasema hayo katika Maadhimisho ya Kutundika Mizinga.  Maadhimisho yaliyofanyika katika Kijiji cha Naikesi Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma akiwakilishwa na mkuu wa wilaya ya songea Joseph Joseph Mkirikiti.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu ameyasema hayo katika Maadhimisho ya Kutundika Mizinga.  Maadhimisho yaliyofanyika katika Kijiji cha Naikesi Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma akiwakilishwa na mkuu wa wilaya ya songea Joseph Joseph Mkirikiti.
 Mkuu wa wilaya ya songea na mkuu wa wilaya Namtumbo wakibadilishana mawazo kuhusu ufugajiwa nyuki
 Wanafunzi wa shule ya secondary Mbunga wa  pokea mradi wa ufugajiwa nyuki
 Kaimu Meneja wa kanda wa huduma za misitu kanda ya kusini Helibeti Haule amesema  wametaka wananchi kutumia njia rafiki za kutunza misitu ikiwemo njia ya  ufugaji wa nyuki,amesema serekari kazi yake ni kutafuta masoko yenye uhakika
 Kanda ya Kusini ikiwa na mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma imeweza kupata Mizinga 5000 kutoka Forest Fund services kanda ya kusini , Mkoa wa Ruvuma umeweza kupata Mizinga  2000, Lindi 1000  na   Mtwara Mizinga 2000.      

Mwalimu wa Miradi Viviani Mwakalonga kutoka Sekondari ya Mbunga yaliko fanyika Madhimisho ya  kutundika Mizinga , amesema ufugaji wa Nyuki katika Shule hiyo utaweza kuongeza huduma ya tiba pamoja na kuongeza lishe kwa wanafunzi .

WANAO TUHUMIWA NA UJANGILI WA KAMATWA SONGEA

 Mratibu Maxmilan Jenes akizumuzia kuhusu ujangili amesema kwa kipindi kifupi shirika lake PAMS FOUNDATION limeshuhudia mizoga ya Tembo zaidi ya 150 wakiwa  wameuwawa na kung`olewa meno 300 yenye thamai zaidi ya milioni 500 jambolinalo sababisha iingizia  hasara kwa serekari.
 Wananchi wa Vijiji vinavyopakana na Mbuga ya Seluu Mkoani Ruvuma wamepongezwa    kwa kuweza kupambana na Ujangiri na kuweza kuwakamata Wawindaji haramu sugu ambao walikuwa wakitafutwa zaidi ya miaka 10 kwa tuhuma za Uwindaji haramu.
 Mratibu wa Shirika la  PAMS FOUNDATION ambalo lina fadhiliwa na Shirika lisilo la kiserikali la  LIZ CLAIBORNE  ART  ORTENBERG  FOUNDATION kutoka Marekani amesema watuhumiwa Yazidu Hassan  Chilombo na mwenzake Said  Milinga hivi karibuni walikuwa katika Mbuga za Seluu walikamatwa na Askari wa wanyamapori    kwa tuhuma za Uwindaji haramu wa Tembo.
 Shirika la PAMS FOUNDATION pamoja na kupambana na Ujangiri likishirikiana na Wananchi, pia linawasaidia wananchi kulinda mazao yao yasiliwe na wanyama waharibifu, , zaidi ya Hekta 1000 za mazao  mbali mbali yame salimika baada Shirika la PAMS FOUNDATION kubuni njia rahisi yakupambana na wanyama wa haribifu kwa kutumia pilipili ,oil chafu pampja na kufuga nyuki ambao ni adui mkubwa wa Tembo 
Mratibu Maxmilan Jenes wa shirika la PAMS FOUNDATION [Shirika linalo jihusisha na kupambana na ujangili liliopo mkoani Ruvuma]  ambalo lina fadhiliwa na  LIZ CLAIBORNE  ART  ORTENBERG  FOUNDATION  amesema watuhumiwa Yazidu Hassan Chilombo na Said Millinga hivi karibuni walikuwa katika Mbuga za Seluu walikamatwa na Askari wa wanyama pori katika doria zao baada ya kukuta wakiwa  wamemuua Tembo ambaye walimng`oa meno yake na kuweza kumkata mkia.

Sunday, March 17, 2013

Friday, March 8, 2013

UHURU KENYATA ASHINDA U RAIS KENYA

UHURU KENYATA AKIWA KATIKA KAMPENI
 Guys im shoo happy wallah and i would like to announce kwamba UHURU KENYATTA ndio Rais mpya wa Kenya.
Kenyatta ameshinda kwa kura 6,173,433 ambayo ni sawa na asilimia 50+1 na kumuacha mbaliii mpinzani wake Raila Odinga.. Matokeo rasmi yatatangazwa kesho saa 5 asubuhi..
From my heart naandika uku machozi ya furaha yananitoka, THIS MAN UHURU KENYATA IS young, wild and free president...i got something to learn from HIM!!
KILA LA KHEIR MR PRESIDENT!!
UHURU KENYATA AKIWAZA KAMPENI, HATIMAYE ASHINDA
MTOTO wa Rais wa kwanza wa Kenya, Marehemu Rais Jomo Kenyatta, ambaye alikuwa anagombea Urais kwa tiketi ya Chama cha TNA, Uhuru Kenyata ameshinda nafasi hiyo baada ya kumwangusha mpinzani wake Raila Odinga.

Hadi saa 8:35 usiku wa leo Uhuru alikuwa mbele kwa kura 6,173,433 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliyekuwa na kura 5, 340,546 ikiwa ni tofauti ya kura 832,887 na majimbo yaliyo kwisha kutangazwa ni 291/291.

Jumla ya kura zote zilizopigwa na kuhesabiwa kwa nafasi ya Urais ni kura 12,338, 667 kutoka katika majimbo yote ya Uchaguzi 291 huku kura zilizoharibika zikiwa 108975 na kura halali zikibaki 12,222,980.

Katika kinyang’anyiro hicho Wycliffe Musalia Mudavadi anashika nafasi ya tatu akiwa amejikusanyia kura 483,981 nafasi ya nne ikienda kwa Peter Kenneth mwenye kura 72,786.

Mgombea wa Alliance for Real Change,Mohamud Abduba Dida anashika nafasi ya tano akiwa na kura 52,848 akifuatiwa na Mwana mama Martha Karua wa National Rainbow Coalition mwenye kura 43,881 hadi sasa.

Nafasi ya saba katika wagombea hao Urais inakwenda kwa James ole Kiyiapi wa Chama cha Restore and Build Kenya ambaye ana kura 40,998 huku nafasi ya ya nane na mwisho ikishikwa na Paul Kibugi Muite wa chama cha Safina
.

Wednesday, March 6, 2013

KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUVUMA YA BAINIWANAFUNZI WALIOFAULU KUSHINDWA KWENDA SHULE

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya  kutafuta Mbinu mwafaka ya kuhakikisha wanafunzi waliofaulu Mtihani wa Darasa la Saba kwenda Kidato cha kwanza wanaripoti Shule walizopangiwa.

Mkoa wa Ruvuma kati ya Wanafunzi 30,555 waliofanya Mtihani wa Darasa la Saba, Wanafunzi 16,578 waliweza kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza lakini walioweza kuripoti na kuanza Masomo ni Wanafunzi 9798 Wanafunzi 6665 hawajaweza kuripoti Shuleni mpaka sasa.
Katibu Msaidizi wa Maadili Kanda ya Kusini Muhuwa Kapangawazi amewataka Viongozi kutekeleza yale waliyo wahaidi Wananchi, hiyo ndiyo itakayo onyesha Maadili mema kwa Wananchi wanao watawala.
Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Ruvuma wameshauri Bajeti zinazotengwa kwa H/za Wilaya  zitangazwe baada ya kufika mikononi mwa Wakurugenzi, kutangaza kabla ya kuwafikia Wakurugenzi ni kuwachonganisha na Wananchi wakidhani Wakurugenzi wamekula Fedha hizo.
Mjumbe wa Ushauri Mkoa wa Ruvuma Jenista Mhagama amesikitika na Mipango inayo kwamisha kufikisha Maendeleo kwa Wananchi, akitoa mfano amesema Banki ya Maji ya Dunia ilitoa kiasi cha Shilingi Milioni 200 mwaka 2003 ili mradi huo utekelezwe kwa kupeleka Maji katika Vijiji vya Maweso lakini mpaka sasa mradi huo haujafanyika.