KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, April 9, 2014

MWILI WA MEJA JENERALI KEVNI GEROLD MSEMWA WAZIKWA KWA HESHIMA ZA KIJESHI MKOANI RUVUMA KWA KUPINGWA MIZINGA 13

Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma aliye kaa chini Mpwapwa akiwa na Bregedia Chacha Nyumani kwa Marehemu Meja Jenerali Kevin Gerold Msemwa
Ili uwe na Kumbukumbu nilazima ushirikishe Vyombo vya Habari Hapo Vyombo vya Habari vya TBC,STAR TV, JESHI  Lenyewa wakichukua kumbukumbu
Maelfu ya Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu walishiriki katika Mazishi ya Maja Jenerali Kevin Gerold Msemwa yaliyofanyika Makaburi ya Mfaranyaki kwa Taratibu za Kijeshi na kupigwa Mizinga 13 ya heshima
Binadamu kwa kawaida haachi Asili Hapo Luteni Jenerali Samweli Ndomba akipokea sakarament katika Maombelezo ya Marehemu Generali Kevin Msemwa
Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Hassani Bendeyeko akitoa salamu za Mwisho kwa Marehemu Kevin Gerold Msemwa Ndumbani kwake Ceedfamer Manspaa ya Songea
Watu mbalimbali wa kitoa Heshima zao hapo Meja Jenerali akitoa Heshima Kwa Marehemu Mejajenerali Kevin Msemwa
Meja Jenerali Kevin Gerold Msemwa ambaye alizaliwa 6/6/1955 Mjini Songea na kusoma Shule ya Msingi Rwanda na Baadaye Sekondari ya Tumainihatimaye alipo jiunga na jeshi la wananchi  . Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika maombelezo na simanzi ya kuondokewa na Meja Jenerali Kevin Gerold Msemwa, walishuhudia Mazishi ya Kijeshi wakati Mizinga 13 ikipigwa kwa heshima yake na taratibu zote za heshima za kijeshi zilifuatwa
Kamati ya Ulinzi Mkoa wa Ruvuma wakitoa heshima kwa Marehemu Kevin Gerord Msemwa
Viongozi waandamizi wa Mkoa wa Ruvuma wakitoa heshima zao kwa Marehemu Kevini Gerold Msemwa
Jeshi ni Jeshi hakuna watu walio na umoja kama Wanajeshi Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza akitoa heshima  kwa marehemu Kevin Gerold Msemwa
Mwili wa Marehemu Kevin Msemwa ukiingia katika Makaburi ya Mfaranyaki Songea Ruvuma
Wanajeshi wakiwa katika kuaga na Kutoa Heshima za Kijeshi Makaburini Mfaranyaki Songea
Usije ukafikiri kuwa hicho ni chuma ,Hiyo ni Wichi ya Kisasa iliyo Tayarishwa kuteremusha Mwili wa Marehemu Kevin Gerold Msemwa Mkanda huo wa Kijani Huvirugiwa kama mikanda ya kwenye lifiti za kupanda na Kushuka
Angalia kwa makini utaona Sanduku likiwa limewekwa kwenye lifuti tayari kwa kuteremushwa chini ya Kaburi
Kanuni za Kijeshi Mwanajeshi anapo Fariki Hununikwa Bendera ya Taifa la Tanzania Pamoja na Kuwekewa Yunifomu alizo kuwa ana Vaa Hapo unaona Viatu ,Kofia,Singe Geneza hili limetengenezwa kwa ufundi wa Hali ya juu kama una jua Vitu vya Vito ungeviona Kama ungeshiri Mazishi haya
Hao ni wanajeshi si Raia wa Kawaida Hapo wapo kikazi zaidi wakitoa Heshima za Mwisho na Kuruhusu Mizinga 13 kupigwa walio na Ugonjwa hawawezi huhudhulia wakati mizinga ikipigwa
Vija wa kike wakijeshi wakitoa Heshima kwa Marehemu Meja Jenerali Kevin Msemwa katika makaburi ya mfaranyaki
Mbwembwe za Kijeshi huziwezi unaona mtindo wa kupumuzika baada ya bendi kutumbuiza

Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Nchini Brigenia Jenerali Kosmas Francis Kayombo akisoma Taarifa kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi Tanzania Generali David Mwamnyange amesema Marehemu Meja Jenerali Kevin Gerold Msemwa alikuwa shujaa wa kuigwa katika Vita vya Kagera yeye ndiye aliyeongoza Kikosi cha Vifaru hadi kumtoa Nduli Idd Amini katika Mipaka ya Tanzania.
 Moja ya mambo ambayo hutia moyo ni kuona Viongozi wakishiriki katika matatizo kufarijiana na wafiwa, hapo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akitoa heshima ya mwisho kwa Marehemu Meja Generali Kevin Gerold Msemwa.
 Uwepo wa Viongozi kwa kujitoa katika msiba ni faraja kwa wananchi wanapoona viongozi wakiungana pamoja na waombolezaji, Hapo ni Mh Gaudens Kayombo Mbunge wa jimbo la Mbinga Mashariki akitoa heshima kwa marehemu
 Brigedia Chacha ni kiongozi wa kijeshi lakini cheo chake hakimfanyi aache imani yake ya dini, Naibu Askofu wa Jimbo Kuu la Songea la Mtakatifu Mathias Mlumba Kalemba Fadha Camilius Haule akimpa mwili wa kristo wakati wa ibada ya maombolezo ya Marehemu Meja Generali Kevin Gerold Msemwa
 Ndugu yangu unaposikia JKT usifikiri ni mchezo vijana hao unaowaona waliweza kuinua mlango wa kaburi (kifuniko) mlango huo ukiwa na uzito wa tani zisizopungua hamsini lakini vijana hao waliweza kubeba kuonyesha moyo waliokuwa nao kwa mkubwa wao wa kijeshi Marehemu Meja Generali Kevin Gerold Msemwa
Picha unayoiona ni ya shujaa wa Kijeshi aliyechangia kumuondoa Nduli Idd Amin Dada katika Vita vya Kagera mara baada ya kuvamia Nchi ya Tanzania, Marehemu Meja Generali Kevin Gerold Msemwa mwaka 1979 aliweza kuongoza kikosi cha Vifaru ambacho kiliwasambaratisha maadui wa Uganda. Mwenyezi Mungu aiweke Mahali pema Roho ya Mrehemu meja Generali kevin Gerold Msemwa.

Naye Meja Denis Devid Kobelo kutoka Makao Makuu ya Jeshi akisoma Wasifu wa Marehemu alimwelezea Meja Jenerali Kevin Gerold Msemwa alivyokuwa mwadilifu na kipenzi cha watu.
Ndugu yangu ona hilo sanduku ukiuliza Bei unaweza Kujenga Nyumba na Ikaisha, Jeshi Mara zite hutoe Heshima zake wakati wa kumzika Mwenzao Wao hawa jali Garama bali Huzingatia Heshima ukitaka kujua Zaidi waulize wana Ruvuima
Inawezekana Toka Mkoa huu ni ingie sijaona Mazishi ya Kijeshi ya liyo Shamiri Heshima zote za kijeshi Hapo wana jeshi wa kiteremusha mili wa Marehemu Kevini Msemwa kwa Wichi ya kisasa iliyo Andaliwa kuteremushia mwili wa Marehemu
Kama huja pitia Mgambo au Jeshi huwezi kuona utamu wake lakini wale walio pitia Jeshi wana jua Utamu wa Maombelezo Hizo ni Heshima za Kijeshi alizo pewa Marehemu Kevin Msemwa
Uwanja wa Mfaranyaki uligeuka kuwa uwanja wa kijeshi hapo Wanajeshi wakitoa Heshima zao za kijeshi kwa Marehemu Meja Jenerali Kevin Msemwa

No comments:

Post a Comment