KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, April 2, 2014

ZANA HARAMU ZA KUVULIA SAMAKI KATIKA ZIWA NYASA ZA TEKETEZWA


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu ametekeza Nyavu za kuvulia Samaki katika wilaya ya Nyasa zinye thamani ya shilingi milioni 87 ili kudhibiti uvuvi Haramu unao sababisha kutoweka kwa samaki wadogo.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akiteketeza Nyavu hiozo amesema serekari haina ugomvi na wavuvi bali serekari ina ugomvi na wavuvi haramu wanao tumia zana haramu kuteketeza viumbe visivyo takiwa kuvuliwa
 Pamoja na kutumia uvuvi haramu bado kuna matumizi mabovu ya Msaada unao tolewa na wahisani rangi ya Blue unayo iona ni Chandarua za Kuzuia Mbu lakini zina tumika kwa ajili ya Uvuvi,Mvuvi yuko tayari kuumwa na Mbu lakini bora apate Samaki

Katika Kuleta Uvuvi wenye Tija Serikali katika Wilaya ya Nyasa imetenga Kiasi cha Shilingi 165,000,000/= ili kununua Ingine mpya za Boti pamoja na Boti zake.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema macho madogo ya nyavu zinapotumika unasababisha kuvua hata Samaki wadogo ambao wangeweza kukufaa hapo baadaye, amewaomba Wavuvi kutumia Zana Bora katika Uvuvi ili kulinda Viumbe ambavyo havistahili kuviangamiza.

Wananchi wa Mwambao wa ziwa Nyasa wameiomba serekari iweze kuwainua ili waweze kuvua uvuvi wa kisasa waepukane na uvuvi haramu ambao wao waliuzoea wakijua ni uvuvi halali

No comments:

Post a Comment